Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MREMBO ALIYEJIOA SASA AMEJIPA TALAKA ANATAKA AOLEWE NA JAMAA


Ni miezi mitatu tu baada ya Cris Galera,33, kugonga vichwa vya habari alipoandaa harusi na kujioa, na sasa anataka kujipa talaka.

Harusi yake ilifanyika Septemba 2021, huku akibadilisha viapo vya ndoa baina yake mwenyewe. 

Daily Star inaripoti kuwa mwanamitindo huyo wa Instagram, sasa anataka kujitaliki akiwa na matumaini ya kuolewa na mpenzi wake mpya. 

Wakati wa harusi yake, Galera alifichua kuwa aliamua kujioa baada ya kuchoshwa na kuvunjwa moyo na wanaume mara nyingi. 

Aliongeza kwamba aliamua kukumbatia upweke na hapana lolote la ajabu kukosekana kwa bwana harusi katika siku yake ya harusi.

Baada ya kubadilishana viapo vya ndoa, Galera alipaga akiwa mwingi wa furaha nje ya Kanisa Katoliki la Sao Paulo, nchini Brazil na koja la maua mkononi. 

Alikuwa amevalia rinda jeupe la harusi, mkufu na kuongezewa mapambo yaliyoanika urembo wake.

 Ataka kujitaliki Takriban siku 90 baadaye, inanoekana Galera amelemewa na upweke sababu ya kuwa katika ndoa pekee yake. Sasa anapania kujipa talaka Hii ni baada ya kupata mtu spesheli ambaye amemfanya kupenda tena. 

"Nilianza kuamini katika mapenzi wakati nilipokutana na mtu mwingine maalum," alisema, akiongeza kuwa alikuwa na furaha wakati "ndoa" yake ilidumu.

Wakati aliulizwa kuhusu uamuzi wake wa kujioa, Galera alisema alifikia katika kipindi fulani maishani mwake ambapo alihisi amekomaa na kuwa mwanamke mwenye bidii.

 Vile vile aliongeza kuwa kwa muda mrefu alikuwa na wasiwasi ya kuishi pekee yake na kutambua kwamba anatakiwa kujifurahisha. Galera alisema kuwa licha ya kufurahia harusi yake na taarifa yake kusambaa, alikataliwa na umma huku wengi wakikosoa uamuzi wake.

Lakini alikataa kubabaishwa na maoni ya wapambe kwa kuwapuuza na kuzingatia maisha yake. "Niliamua kwamba sitasoma tena maoni ya chuki. Maoni ya watu hayatabadilisha kile ninachofikiria au kuongeza chochote," alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com