AKIBA BENKI YAZINDUA KAMPENI "TUPO MTAANI KWAKO"



Na Mwandishi wetu- Dar es salaam

Taasisi za kifedha hazina budi kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Wananchi kwa kuwasogezea karibu ili kusaidia kupunguza adha ya kutumia muda mwingi kufuata huduma umbali mrefu na kuchelewa kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Wito huo ameutoa Septemba 21, 2024 Dar es salaam Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo Biashara Benki ya Akiba, Danford Muyango wakati akizindua rasmi kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” katika tawi la Kijitonyama la benki hiyo , Letsya Tower ambapo amesema wapo mtaani kila mahali wakitoa huduma ikiwemo elimu ya mikopo, jinsi ya kutumia huduma za kidigital VISA card,ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking.
"Tumezindua rasmi program yetu ya TUPO MTAANI KWAKO kupitia timu yetu bobezi ya mauzo sasa tunakufika popote ulipo nchi nzima kupitia timu yetu ya mauzo kupata huduma zetu za kufungua akaunti , elimu ya mikopo pamoja na jinsi ya kutumia huduma zetu za kidijitali za VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking", amesema Afisa biashara

Muyango amesema Program hiyo inaenda sambamba na kampeni ya Road show ya kutoa utambulisho kwa timu ya “Tupo Mtaani kwako” katika vitongoji na mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post