Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiimba pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Chief Zulu kuhusu matumizi ya Computer shuleni hapo, Songea mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Shule ya Awali na Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Chief Zulu, Songea Mkoani Ruvuma
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Septemba 24,2024 Mhe. Rais Samia amesema:
“Nimeambiwa shule hii ni ya mchepuo wa Kingereza. Sasa nina pendekezo. Unajua unapobadilisha mitaala ya elimu, Waziri wa Elimu yuko hapa. Tumebadilisha mitaala ya elimu na sera yetu ya elimu kuendana na mabadiliko ya Dunia yanavyokwenda. Shule hii ni mchepuo wa watoto ambao watafundishwa kwa Kingereza. Kwa hiyo tunatarajia watakapotoka hapa huko njiani ni ‘how are you’, ‘how are you doing’na hivyo na mambo kama hayo”.
“Katibu wangu ananiambia hapa kuna shida ya bwalo la chakula. Na gharama yake ni Sh Milioni 200. Sasa Halmashauri mmekauka kweli? Bwana Meya na Mkurugenzi wa Halmashauri mmekauka kweli 200 ya bwalo haipo. Sasa tufanye hivi, nyie toeni 100 na mimi natoa 100. Sawa, ili tujenge bwalo haraka watoto wale kwenye bwalo na wafundishwe vizuri tabia za kula kwenye bwalo halisi la kulia”,amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Chief Zulu, Teofilo Mbunda kuhusu matumizi ya Computer shuleni hapo, Songea mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua moja ya Madarasa ya Shule ya Awali na Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Chief Zulu, mara baada ya ufunguzi mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024.
Social Plugin