Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAFUNZI 45,693 KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU LA 7 SHINYANGA


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

WANAFUNZI 45,693 mkoani Shinyanga, wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya darasa la saba, huku Mkuu wa mkoa huo Anamringi Macha, akionya udanganyifu kwenye mitihani hiyo.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 10,2024 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema mitihani ya kuhitimu elimu ya darasa la 7 itafanyika kuanzia kesho na kuhitimishwa kesho kutwa kwa nchi nzima, na kwamba wanafunzi 45.693 mkoani humo watafanya mtihani huo, wavulana ni 19,528 na wasichana 26,165, huku akionya kutofanyika udanganyifu wa mitihani, na kwamba kwa shule za binafsi ambazo zitagundulika kufanya udanganyifu huo zitafungiwa.

“shule za ‘private’ zinatatizo moja zina ushindani, mimi ushindani huo sina tatizo, hata shule za serikali zina ushindani lakini shughuli hizo wanatenda haki kwa shule nyingi, ila binafsi wana mahanghaiko ya kutaka watoto wafaulu kama sehemu ya kuitangaza shule, na hivyo baadhi ya shule hujiingiza kwenye udanganyifu wa mitihani, na shule itakayogundulika tutaifungia,”amesema Macha.

“kwa upande wa shule za serikali itakayobainika kufanya undanganyifu, hatua itachukuliwa na hasa kwa walimu, tusishindane kwa kuwafanyia undanganyifu watoto, tuwaache waonyeshe ukweli kwa kile ambacho wamejifunza ndani ya miaka saba,”ameongeza.

Amewaonya pia wazazi nao wasije wakajiingiza kwenye udanganyifu huo wa mitihani,pamoja na wanafunzi wasikubali kupewa vikaratasi vya majibu, huku akiwasisitiza wasiwarubuni watoto wao kufanya vibaya kwenye mitihani hiyo, kwa lengo la kupata wachungaji wa mifugo, na watoto wa kike kupata fursa ya kuwaozesha ndoa za utotoni.

Aidha, amesema maandalizi ya mtihani huo yamekamilika na wanafunzi 45,693 mkoani humo wanatarajia kufanya mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi, wavulana 19,528 na wasichana 26,165, na kwamba walimu watakao simamia mitihani hiyo ni 3,339.

Nao baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba ambao wanatarajia kufanya mitihani akiwamo Mariamu Amosi wa shule ya msingi Mwenge, alisema wamejiandaa vizuri kufanya mitihani hiyo na watapata ufaulu mzuri.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com