MWONGOZO WA USHIRIKI WA WANAUME KATIKA AFYA YA UZAZI WAWAKUTANISHA WADAU KISHAPU


Mwezeshaji kitaifa wa masuala ya afya ya uzazi Dkt.Tarama Ndosi akizungumzia mwongozo wa ushiriki wa wanaume katika afya ya mama baba na mtoto 


Na Sumai Salum - Kishapu

Ofisi ya Rais -TAMISEMI,Wizara ya Afya kwa kushirikiana na asasi ya kiraia TMEPid kwa ufadhili wa UNFPA wamewakutanisha wadau wa afya ngazi ya wilaya na mkoa,viongozi wa dini,wafanyakazi Watoa huduma katika vituo na ngazi ya jamii,dawati la jinsia polisi na magereza pamoja na watu wenye ulemavu Mkoani Shinyanga ili kutoa maoni ya kuboresha mwongozo huo.

Akizungumza wakati akiwasilisha mada Mwezeshaji kitaifa wa masuala ya Afya ya Uzazi Dkt .Tarama Ndosi leo Septemba 19,2024  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga amesema lengo ni kuelezea mwongozo wa ushirikishwaji wanaume katika huduma ya afya ya uzazi katika makundi hayo.

"Wizara yetu ya afya na Ofisi ya Rais-TAMISEMI imekusudia kukusanya maoni ya wadau kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu ilikufanya maboresho ya mwongozo huo kutokana na wanaume kuwa nyuma katika suala la afya ya uzazi", amesema Dkt. Ndosi.

Aidha ameongeza  kuwa wanaume wa jamii ya ki Afrika kutokana na mila na desturi zilizopita wakati zimewafanya baadhi yao kuwa nyuma katika masuala ya afya ya uzazi jambo linalosababisha kutokuwepo na usawa katika kutoa maamuzi ya  huduma ya afya ya uzazi.

Aidha ameongeza kuwa  mwongozo huo utaboreshwa kutokana na maoni ya wadau na pia itasaidia kuondoa unyanyapaa,ukatili wa kijinsia,kuleta usawa katika kutoa maamuzi kwa baba na mama kuamua kuhusu masuala yote ya uzazi" ameongeza Dr.Ndosi

"Wizara inaelekeza mama aendapo kuanza kliniki aende na mume wake ili wachunguzwe wote afya zao ila wanaume hawakotayari na kuona ni wajibu wa mama peke yake hata ufikapo wakati wa mama kujifungua ikihitajika vifaa hayuko tayari kutoa fedha ya kununua vifaa vyote hitajika tunatakiwa kuhama kwenye mfumo huo na Sisi wanaume kutambua kuwa tunapaswa kushiriki katika masuala yote ya afya ya uzazi tukiwa ni wazazi kamili wa watoto wetu", ameongeza Dkt. Ndosi

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw. Elikana Zabron amepongeza uwepo wa mwongozo huo kwani utaondoa mfumo dume huku akiwataka wadau wote wa afya kutoa elimu kwa jamii ili wanaume washiriki kikamilifu katika malezi ya pamoja ya mtoto.
Mwezeshaji kitaifa wa masuala ya afya ya uzazi Dkt.Tarama Ndosi akizungumzia mwongozo wa ushiriki wa wanaume katika afya ya mama baba na mtoto 
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ,Elikana Zabron akizungumza kwenye kikao cha uwasilishaji mwongozo wa ushiriki wa wanaume katika afya ya mama baba na mtoto 
Mganga mkuu  Mkoa Shinyanga   Dr.Yudas Ndugile akizungumza leo Septemba 19,2024 kwenye kikao cha uwasilishaji mwongozo wa ushiriki wa wanaume katika afya ya mama baba na mtoto kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga  Dkt. Bahati Joseph akizungumza kwenye kikao cha uwasilishaji mwongozo wa ushiriki wa wanaume katika afya ya mama baba na mtoto 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post