Na Mwandishi wetu
Ameeleza kuwa, ni muhimu kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuachana na siasa za upotoshaji na kumpongeza Rais Samia kwa juhudi kubwa anazozifanya kwa maslahi ya taifa.
Magari amesema "Nyinyi majirani zetu mlikuwa hamna ofisi kwa takribani miaka 30, leo Mama kajitahidi katoa fungu kawahamishieni ofisi na kupelekwa Mikocheni mnataka nini majirani?"
Aidha Magari amewataka CHADEMA kumuunga mkono Rais Samia kwa kutengeneza mazingira bora ya kuvutia wawekezaji na ya kufanyia biashara nchini.
“Mnasema nchi haina amani, ni amani gani mnayoitaka? Wawekezaji wamerudi, watu wanafanya wanachotaka,hata nyie mnaongea mnachojisikia, hiyo siyo amani? . Mama anafanya kazi kubwa, ameshughulikia umeme, maji, treni ya umeme, barabara kujengwa kwa viwango na viwanda, mpeni Rais Samia maua yake kwani anafanya mengi kwenye hii nchi”
“Mkikaa kwenye vikao vyenu kuweni wakweli kwamba mama Samia ndiyo kila kitu, apewe mitano yake na akija tena apewe mitano mingine jumla 10, huyu mama ndiyo aliyeweza kuiongoza hii nchi” ,amesisitiza
Social Plugin