Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA : UTUMISHI WETU MIMI NA NYINYI NI KUHUDUMIA WANANCHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga mkoani Ruvuma tarehe 25 Septemba, 2024.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia amesema: "Ndugu zangu wa Mbinga, serikali imeendelea kuleta fedha nyingi kama ilivyotajwa hapa na waheshimiwa wabunge kwa ajili ya maendeleo na huduma za jamii.  Kwa jamii yetu iliyopo hapa Halmashauri ya wilaya Mbinga. Hivyo niwatake watendaji wote kusimamia miradi na watendaji ni pamoja na madiwani muendelee kuweka nguvu kusimamia miradi ili yale yanayowakera wananchi yaweze kuondoka. Utumishi wetu, mimi na nyinyi ni kuhudumia wananchi. Sisi ni watumishi wa wananchi na si mabwana wa wananchi"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com