Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na kauli zinazotia mashaka kwa wananchi juu ya matukio ya kupotea kwa watu.
Watu wengi wamekuwa wakihusisha na kulituhumu jeshi la Polisi bila kufanya uchunguzi wa kina ikiwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuwa kikitoa madai kuwa wanachama na wafuasi wake kadhaa wametekwa na serikali.
Ni muhimu kwa umma kuelewa kwamba serikali ina jukumu la kuhakikisha usalama wa raia na kushughulikia vitendo vyote vya uhalifu bila kujali itikadi za kisiasa za wahusika.
Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kulinda sheria na usalama wa nchi bila kubagua na itachukua hatua stahiki dhidi ya yeyote anayejiingiza katika shughuli za kihalifu bila kujali ni chama gani cha siasa anachotoka.