Wajasiriamali 150 kutoka wilaya za Kahama,Nyang’hwale na Msalala wamehitimu mafunzo ya siku 10 ya biashara kupitia Kupitia Programu ya Kuendeleza Biashara za Wazawa (Local Business Development Program) inayotekelezwa na Mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, yaliyolenga kuwajengea uwezo na kuwasaidia waweze kunufaika na fursa zilizopo kwenye sekta ya madini.
Mahafali ya kuhitimu mafunzo hayo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Kitapela,Kakola na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa wakiwemo wakufunzi, Maafisa wa Serikali, Taasisi za Kifedha na mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Nyang'wale Mhe. Grace Kingalame.
Akiongea na wahitimu kabla ya kuwakabidhi vyeti vya kuhitimu mafunzo,Kingalame alipongeza mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuandaa mafunzo hayo na aliwataka Kutumia maarifa waliyoyapata Kuleta mabadiliko chanya katika biashara zao sambamba na kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo katika sekta ya madini hususani katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu na makampuni mengine yaliyopo katika ukanda huo.
Alisema mafunzo haya yaliyoandaliwa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu yamefanyika kwa wakati mwafaka ambao mbali na kulenga kuwawezesha wajasiriamali kuchangamkia sekta zilizopo katika sekta ya madini pia Serikali imetenga mikopo mingi kwa ajili yao ambapo ili kunufaika nayo ni muhimu kupatiwa mafunzo ya kibiashara ili Wale watakaopata Mikopo waweze kuirejesha kwa wakati.
Awali Akiongea kwa Niaba ya Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulaynhulu, Abdallah Kipara, alisema Mgodi Umeweka Kipaumbele katika kuhakikisha mipango ya Serikali inayolenga jamii inafanyika kwa ushirikiano mkubwa na wadau wote kwa kuamini kwamba mafanikio ya mgodi yatakuwa Endelevu ikiwa yatachochea na kuchangia katika kuboresha maisha ya wanajamii wanaotuzunguka.
“Tunajivunia kwa kuongoza njia kwa kufanikiwa kuendesha program hii ya maendeleo ya biashara kwenye maeneo yanayozunguka migodi na tumetimiza wajibu zaidi ya sheria ya maudhui ya ndani (Local content) na tutaendelea kuunga mkono maendeleo ya kampuni ndogo na za kati ambazo ni muhimu sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi,” alisema Kipara.
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Mafunzo hayo walisema fursa ya mafunzo hayo waliyoyapata yatawasaidia kukuza biashara zao sambamba na kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara ili kuendana na teknolojia na masoko ya kisasa .
Wajasiarimali 150 waliohitimu mafunzo hayo walitunukiwa vyeti vya ushiriki.
Mwakilishi wa Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulaynhulu, Abdallah Kipara
Kaimu Meneja kitengo cha Mahusiano ya Jamii na Mazingira Zuwena Senkondo
Baadhi ya wahitimu wakipokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi
Baadhi ya wahitimu wakipokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi
Baadhi ya wahitimu wakipokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick katika hafla hiyo
Social Plugin