Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mkutano na Rais wa China, Xi Jinping pamoja na ujumbe wake mapema leo katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing.
Rais Samia amefanikiwa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ya Tanzania na nchi muhimu duniani ikiwepo China tangu alipoingia madarakani Mwaka 2021.
Kwa Mwaka huu wa 2024 Rais Samia na Xi Jinping wamejadiliana kuimarisha uhusiano wetu mzuri uliodumu zaidi ya miaka 60.
Vilevile baada ya kikao hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema walishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA.
Social Plugin