WANANCHI TUMULI NA IGUGUNO WAHAMASISHWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos amewataka wakazi wa kata za Tumuli na Iguguno wilayani hapa kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa utakaoufanyika Novemba 27,2024

Wito huo ameutoa Septemba 9,2024 wakati wa ziara ya kikazi ya kata kwa kata yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wakazi wa kata hizo.

“Tujitokeze kwa wingi kuwania nafasi za Uongozi lakini pia tujitokeze kwa wingi kwenye mikutano ya siasa ili tuweze kusikiliza sera za viongozi wetu tunaotaka kuwachagua, na itakapofika Novemba 27, 2024 ukapige kura kumchagua kiongozi unayemtaka.” DED Asia Messos

Vile vile amesisitiza juu ya kuchagua viongozi makini wazalendo wenye kiu ya kuleta maendeleo kwa wananchi na si wabinafsi, “Lakini tunapoenda kuchagua viongozi wetu, tusichague ili mradi tumechagua, chagueni viongzi wenye shahuku ya kuleta maendeleo” DED Asia Messos

Akizungumzia kuhusu zoezi la kuandikisha wapiga kura, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Asia Messos amesema mchakato wa kuandika wapiga Kura kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura utaanza Oktoba 11-21,2024 na kuwataka wananchi wajitokeze kujiandikisha katika daftari hilo.

“Ili uweze kupiga kura unapaswa uwe umejiandikisha kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura, mchakato huu utaanza Tarehe 11-20, Oktoba 2024, itakapofika hii tarehe twendeni kwa pamoja tukajiandikishe tupate nafasi ya kuchagua viongozi wetu tunaowataka” Bi. Asia Messos

Aidha Bi. Asia Messos amewakumbusha wakazi wa kata hizo juu ya umuhimu wa kulinda miundombinu ya serikali, kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, kuhakikisha wanashiriki katika shughuli za maendeleo pamoja na kuchangia chakula shuleni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post