Na Christina Cosmas, Morogoro
Kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi, Askari Polisi Mkoa wa Morogoro wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalum katika kituo cha kulelea watoto yatima cha MEHAYO kilichopo Mazimbu mkoani humo.
Aidha, akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Alex Mkama ameitaka jamii kuendelea kuwasaidia watu wenye uhitaji hususani watoto yatima ili nao wajione ni sehemu ya jamii yenye kupendwa na kuthaminiwa.
Kamanda Mkama aliambatana na askari wa vyeo mbalimbali na kukabidhi msaada kwa watoto hao ikiwa ni sehemu ya majitoleo yao na hasa kuguswa na kundi hilo lenye uhitaji kwenye jamii.
Social Plugin