Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIJANA AGONGWA NA TRENI AKITOKA KUNYWA POMBE SHINYANGA


Kijana aliyejulikana kwa jina la Juma Malale (26) mkazi wa Ndembezi Manispaa ya Shinyanga amefariki dunia baada ya kugongwa na Treni.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi Septemba 14,2024 katika eneo la Ubalaji Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa mtu huyo alikuwa ametoka kunywa pombe akalala relini wakati akielekea nyumbani na baada ya treni kufika hapo ilipiga honi lakini hatutoka relini hivyo ajali hiyo ikatokea kutokana na kwamba Treni huwa haisimami.

Hata hivyo bado sababu za kujiua za Juma Malale ambaye alikuwa anajishughulisha na ujenzi wa nyumba hazijajulikana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com