WATENDAJI KISHAPU WATAKIWA KUTUMIA VIZURI PIKIPIKI ZA SERIKALI, KUHAMASISHA KILIMO CHA PAMBA


Kaimu katibu tawala Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw. Fadhili Mvanga (Kushoto) akikabidhi namba za pikipiki mtendaji wa kata ya Lagana( kulia) leo Septemba 19,2024 kwa ajili ya ufuatiliaji na utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kata. Picha na Sumai Salum
Kaimu katibu tawala Wilaya ya Kishapu Mkoani ShinyangaBw.Fadhili Mvanga (Kushoto) akikabidhi namba za pikipiki mtendaji wa kata ya Mondo Ndoto Nyama (kulia) leo Septemba 19,2024 kwa ajili ya ufuatiliaji na utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kata.
Kaimu katibu tawala Wilaya ya Kishapu Mkoani ShinyangaBw.Fadhili Mvanga (Kushoto) akikabidhi namba za pikipiki mtendaji wa kata ya Bubiki Hapi Shonde (kulia) leo Septemba 19,2024 kwa ajili ya ufuatiliaji na utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo ya Kata.
Na Sumai Salum - Kishapu

Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga , Fadhili Mvanga amewaonya watendaji wa serikali waliopewa pikipiki na serikali ya awamu ya sita  inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wazitumie kwa kazi zilizokusudiwa na serikali na nidhamu ya hali ya juu.

Ameyasema hayo leo Septemba 19,2024 katika ofsi za Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakati akikabidhi pikipiki hizo kwa watendaji wa kata tatu(3) Lagana,Mondo pamoja na Bubiki.

"Pikipiki hizi mhakikishe zinasaidia Kuibua vyanzo vipya vya mapato,kusimamia mapato vizuri,ufuatiliaji na kusimamia miradi ya maendeleo na kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi msizifanye kuwa za biashara na matumizi yenu binafsi", amesema Mvanga

Mvanga amewataka watendaji hao kuhakikisha wanatekeleza shighuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na uhamasishaji wananchi kulima kilimo cha pamba chenye tija ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja,jamii,halmashauri,na nchi kwa ujumla wakishirikiana na maafisa kilimo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Elikana Zabron ameipongeza serikali ya awamu ya sita huku akisema pikipiki hizo zitawasaidia watendaji wa Kata kuongeza mapato ya Halmashauri  kutokana na urahisi wa  ukusanyaji kodi kuwa wa uhakika sambamba na kufuatilia shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.

Aidha mtendaji wa Kata ya Lagana Kashinje Ikombe baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo kwa niaba ya watendaji ameahidi kutumia kwa kazi maalumu iliyokusudiwa na serikali.
Kaimu katibu tawala Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Fadhili Mvanga akizungumza leo Septemba 19,2024 na watendaji wa Kata za Lagana, Mondo na Bubiki wakati akikabidhi pikipiki zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita kwa lengo la urahishishaji utekelezaji shughuli  mbalimbali  maendeleo katika maeneo yao
Kaimu Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw. Elikana Zabron akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki zilizotolewa na serikali kwa kata ya Lagana,Mondo na Bubiki leo septemba 19,2024 kwenye viwanja vya Halmashauri hiyo kwa lengo la utekelezaji shighuli za  maendeleo kwenye kata zao.
Mtendaji wa Kata ya Lagana Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Kashinje Ikombe akizungumza Leo Septemba 19,2024 baada ya kukabidhiwa pikipiki zenye lengo la utekelezaji shughuli za maendeleo ya kata na Kaimu katibu tawala wa Halmashauri hiyo Bw. Fadhili Mvangi kwenye viwanja vya halmashauri hiyo




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post