Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (aliyevaa miwani)akizindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amezindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola yenye urefu wa Km 73 ikiwa ni utekelezaji wa ushauri wake wa kuanza kutumia Lugha ya Kiswahili katika Mabango yote ya miradi ndani ya Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo Jumatatu Septemba 23,2024 Mhe. Macha amesema Lugha ya Kiswahili inatumiwa na wananchi wengi na kwa kuwa miradi yote ni ya wananchi hivyo wanapaswa kuelewa nini kimeandikwa na nini kinatekelezwa na Serikali katika maeneo yao.
“Nawapongeza TANROADS kutayarisha na kuweka bango hili kwenye mradi wa ujenzi wa Kilometa 73 ya Kahama hadi Kakola kwa kiwango cha Lami ukaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 101 .2. Hili ni bango la Kwanza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili katika Mkoa wa Shinyanga. Naagiza pia kwenye maeneo mengine miradi sekta mbalimbali mabango yaandikwe kwa Lugha ya Kiswahili, hata kama mtaweka Bango la Kiingereza lakini pia muweke la Kiswahili kwani Lugha ya Kiswahili inajitosheleza kwa kila kitu”,ameeleza Mhe. Anamringi.
"Nawapongeza sana Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga chini ya Mhandisi Samwel Joel Mwambungu kwa kuwa wa kwanza kutekeleza ushauri wangu wa kuanza kutumia Lugha ya Kiswahili katika mabango yote yanayoelezea miradi inayotekelezwa kwa wananchi ndani ya Mkoa wa Shinyanga, hongera sana Meneja Mhandisi Mwambungu," amesema Mhe. Macha.
Ameeleza kuwa, kuanza kutumika kwa Lugha ya Kiswahili katika mabango ya miradi inasaidia wananchi kuelewa kinachoendelea katika miradi yote ya maendeleo kwa wananchi ambao ni wengi zaidi na ambao ndiyo wenye miradi hiyo ikiwa pia ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Kiswahili ni Lugha yetu, lazima tufaidike na maelezo ya Kiswahili katika miradi kwa sababu miradi mingi imeandikwa kwa Lugha ya Kiingereza tunataka wananchi waelewe kazi zinazofanywa na Serikali , waelewe miradi inahusu nini lakini pia huu ni utaratibu wa kuenzi, kutunza na kudumisha matumizi ya Lugha ya Kiswahili katika maeneo yote”,ameongeza Mhe. Macha.
Katika hatua nyingine ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Kahama – Kakola huku akiipongeza TANROADS Mkoa wa Shinyanga pamoja na Mkandarasi kwa namna walivyojipanga kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
“Nimeridhika na kasi mnayoendelea nayo, nimeona mitambo ni mingi, wito wangu hakikisheni mnaongeza kasi zaidi ili wananchi waanze kutumia barabara hii muhimu ambayo inaunganisha mkoa wa Geita na Shinyanga lakini pia inachangia kukuza uchumi wa mikoa hii nan chi kwa ujumla”,amesema Mhe. Macha.
Kwa upande Meneja Mradi wa ujenzi wa barabara hiyo kupitia Kampuni ya Ukandarasi ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) bw. Chen Yang amesema ujenzi unaendelea vizuri na mpaka sasa hawajapata changamoto yoyote huku akiahidi kukamilisha ujenzi ndani ya muda uliopangwa.
Shughuli za ujenzi zikiendelea katika Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samwel Joel Mwambungu amesema barabara ya Kahama- Bulyanhulu JCT – Kakola yenye urefu wa Kilomita 73 ni barabara ya Mkoa inayounganisha Mji wa Kahama na Mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu Gold Mine’ inajengwa kwa kiwango cha lami ikiwa ni moja ya mikakati ya serikali kuharakisha maendeleo ya uchumi na kijamii Mkoani Shinyanga.
Amesema ujenzi wa barabara hiyo unafadhiliwa kwa asilimia 100% na mgodi wa Barrick Bulyanhulu Gold Mine kupitia Wizara ya Ujenzi na TANROADS inayosimamia utekelezaji ambapo Mkandarasi ni China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) mhandisi Mshauri ni TANROADS Engineering Consulting Unit (TECU) ukitekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 101.2 kazi ya ujenzi imeanza Juni 3,2024 ukitarajiwa kukamilika Septemba 4,2024.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akizindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akisoma maandishi wakati akizindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akizindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akizindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza baada ya kuzindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akikagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
eneja Mradi wa ujenzi wa barabara hiyo kupitia Kampuni ya Ukandarasi ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) bw. Chen Yang akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akikagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samwel Joel Mwambungu akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akikagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samwel Joel Mwambungu akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akikagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samwel Joel Mwambungu akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akikagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Shughuli za ujenzi zikiendelea katika Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Shughuli za ujenzi zikiendelea katika Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Shughuli za ujenzi zikiendelea katika Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Shughuli za ujenzi zikiendelea katika Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog