Mtu mmoja aliyehafamika kwa jina la Kumalija Kandondoge anayekadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 50 mkazi wa kata ya Mwime Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga anashikiliwa na Jeshi la Polisi pamoja na jeneza lake alilokutwa nalo nyumbani kwake.
Hata hivyo, Kumalija Kandondoge amekana kumiliki wa jeneza hilo na kudai kuwa lilikuwa ni la mmoja ya msanii wa nyimbo za asili aliyeliacha nyumbani hapo.
Wakazi na majirani wa eneo hilo walijawa na hofu baada ya kukatazwa na bwana Kumalija kupita au kusogea kwenye eneo la pembezoni mwa nyumba yake alipokuwa amehifadhi jeneza hilo.
Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga ACP. Kennedy Mgani amethibitisha kumshikilia bwana Kumalija pamoja jeneza lake huku akibainisha sababu zilizopelekea mtu huyo kuishi na jeneza ni kutokana na changamoto ya afya ya akili inayomkabili inayosababishwa na msongo wa mawazo kutokana na kutengwa na familia yake kwa muda mrefu.
"Ni kweli mtu hiyo alikwenda kujichongea jeneza na kulipeleka kwenye makazi yake tulipofanya uchunguzi tulibaini kuwa mtu huyu alikuwa na msongo wa mawazo iliyompelekea changamoto ya afya ya akili kutokana na kutengwa na familia yake kwa muda mrefu",amesema ACP Mgani.
Social Plugin