Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewahimiza Wafanyabiashara walipe kodi stahiki na kuwasilisha marejesho ya kodi kwa wakati ili kuepuka adhabu na riba endapo watachelewa.
Wito huo umetoewa leo Jumatano Septemba 25,2024 na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi wakati wa kikao chake na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga chenye lengo la kupokea maoni, kero na changamoto za wafanyabiashara.
“Ni wajibu wako kuzingatia tarehe za kulipa kodi stahiki bila nyongeza yoyote kwa wakati, unatakiwa kulipa kodi unayostahili wafanyabiashara, mna wajibu wa kuwasilisha marejesho ya kodi kwa wakati, kodi ikichelewa kulipwa ina riba. Tambua tarehe za kuwasilisha Return na lipa kodi kwa wakati, ukileta umechelewa kuna adhabu na riba”,amesema Mrengi.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi akizungumza na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga
Katika hatua nyingine amesema TRA inaendelea kwenda kwenye maeneo wanakofanyia biashara walipa kodi ili kuwasogezea karibu huduma.
Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Josephat Mwaipaja amewashukuru Wafanyabiashara mkoani Shinyanga kwa kuendelea kuwa walipa kodi wazuri.
Amewasihi wafanyabiashara pindi wanapokutana na changamoto wawasiliane na maafisa wa TRA ili kutatua kero zao na kuwaomba watumie siku ya Alhamisi kukutana na TRA
Naye Kaimu Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Shinyanga Khatibu Mgeja ameishukuru TRA kwa kuendelea kutoa fursa ya kukutana na wafanyabiashara ili kutoa maoni huku akiwahamasisha wafanyabiashara kujenga utamaduni wa kufika TRA kueleza kero na changamoto zao badala ya kukaa kimya.
Mbali na kuishukuru TRA kwa kuendelea kutoa elimu mara kwa mara wameomba kuwe Mfumo wa kufanya malipo na mawasiliano na TRA kwa njia ya mtandao na wapewe Namba ya malipo (Control number) ya kulipa mara moja kwa mwaka badala ya kulipa kwa awamu na kulazimika kwenda TRA mara kwa mara.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi akizungumza leo Jumatano Septemba 25,2024 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga wakati wa kikao chake na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga chenye lengo la kupokea maoni, kero na changamoto za wafanyabiashara. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi akizungumza leo Jumatano Septemba 25,2024 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga wakati wa kikao chake na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga chenye lengo la kupokea maoni, kero na changamoto za wafanyabiashara.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Josephat Mwaipaja akizungumza kwenye kikao cha Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga

Kaimu Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Shinyanga Khatibu Mgeja akizungumza kwenye kikao cha Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga

Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga wakiwa ukumbini
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga
Mfanyabiashara akichangia hoja kwenye kikao cha Kamishina wa Kodi za Ndani TRA, Alfred Mrengi na Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga
Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara mkoa wa Kikodi Shinyanga wakiwa ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog