UJENZI WA KISIMA KIREFU MKOMBOZI KWA WANAFUNZI WENYE UMRI MDOGO SHULE YA MSINGI NYAGISESE


Na Frankius Cleophace - Tarime Mara.

Wanafunzi wa shule ya msingi Nyagisese Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya upatikani wa maji safi na salama shuleni hapo jambo ambalo linatajwa kuchangia utoro kwa wanafunzi pamoja na magonjwa ya matumbo hususani kwa wanafunzi wenye umri mdogo.

Shrika la Living For Other lililopo wilayani Tarime Mkoani Mara kwa kuliona hilo limeachimba kisima kirefu maeneo ya shule hiyo nakukikabidhi ili kiweze kusaidia jamii wakiwemo wanafunzi wa shule ya msingi Nyagesese kata ya Nyandoto Halmashuari ya mji wa Tarime
 
 Akiongea wakati wa kukabidhi kisima hicho Kilichogaharimu zaidi ya Milioni 17 Anasitazi Mwita Mkazi wa Nyagisese  amesema kuwa kabla ya kuwepo  kwa kisima hicho walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata maji  na kipindi cha Mvua Mto Mori unajaa na maji yanakuwa machafu kutokana na tope.

“Asubihi tulikuwa tunaamusha watoto wetu mapema kwenda kuchota maji mto Mori wanachelewa kwenda shule wanapigwa na walimu wao  na kuopigwa ni moja ya ukatili sababu wengine walikuwa wanaogopa kwenda shule hivyo hiki kisima sasa ni mkombozi kwetu kitapunguza utoro kwa wanafunzi hawa” alisema Anasitazia.

Anasitazia aliongeaza kuwa wakati mwingine watoto wadogo kuanzia darasa la awali la kwanza mpaka la tatu kwa sababu bado ni wadogo walikuwa wakinywa maji ya Mto mori ambayo hayajachemushwa siyo mazuri kwa afya yanaweza sababisha magonjwa ya matumbo hivyo  uwepo wa kisima hicho sasa ni mkombozi kwao.

Kwa upande wake Isack Justin Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Living For Others alisema kuwa kupitia wafadhili mbalimbali wamekuwa wakisaidia jamii yenye mahitaji na hicho ni kisima cha pili kujengwa kwa ajili ya kusaidia jamii yenye mahitaji.

 Aizak amesisitiza sasa wananchi kutunza kisima hicho ili kiendelee kuhudumia jamii hiyo ya Nyagisese kata ya Nyandoto Halamashauri ya mji wa Tarime mkoani Mara.

Leah Moses ni Afisa Maendeleo kata ya Nyandoto aliongeza kuwa mtaa huo ulikuwa unakumbwa na changamoto ya  hukosefu wa maji nakueleza kuwa jamii imekuwa ikikumbwa na Magonjwa ya Matumbo wakiwemo watoto wadogo pamoja na utoro shuleni pale wazazi wanapokuwa mashambani watoto ndio wanachukua jukumu la kutafuta maji.

 “Wazazi wengi huku ni wakulima hivyo wanapokuwa shambani watoto ndio wanachukua jukumu  la kuchota maji kupitia mito nawakati wa mvua, mito na madimbwi inajaa jambo ambalo ni hatari pia kwa watoto hao wanaweza kutumbukia kwa bahati mbaya” Alisema Leah.

 Chacha Mwita ni mkazi wa Nyagisese ametoa shukrani kwa msaada huo nakuhaidi sasa kutunza kisima hicho kwa ili kiendelee kutoa huduma kwenye jamii.

Naye Ghati Okoth ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya mji wa Tarime laisema kuwa Ustawi wa jamii wakiwemo watoto unahitaji Afya, pamoja na maji Safi na Salama hivyo sasa kupatikana  kwa maji hayo itasaidia usafi kwa akina mama hao pamoja na watoto hao kuoga mara kwa mara ili kuepusha maradhi ya mara kwa mara.

“Sisi kama serikali tunatambua kazi za mashirika tunaomba waendelee kujitoa kwa ajili ya jamii yenye mahitaji” alisema  Ghati.

 Ghati aliongeza kuwa amekuwa akipokea taarifa zinazhusu masuala la ndoa kutaka kuvunjika kwa sababu na akina mama kuamka asubuhi mapema sana kwenda kuchota maji  maeneo ya mbali hivyo sasa kupitia kisima hicho sasa wenda changamoto hizo zikapungua ambazo wakati mwingine zilikuwa zinapeleea Ukatili vikiwemp vipigo kwa wanawake wanapochelewa mtoni.

Kwa mujibu wa Takwimu za Taifa za Makisio ya Idadi ya Watu zilizotolewa na Idara ya Takwimu ya Taifa, Tanzania ina takribani watoto 16,524,201 (wavulana 8,328,142 na wasichana 8,196,056) wenye umri wa miaka 0 – 8 (ambao ni 30% ya watu wote)hii inamaanisha kuwa katika kila watu watatu, kuna mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 0 – 8. Kundi hili la watoto wadogo linahitaji kuangaliwa kwa karibu na kufanyiwa uwekezaji ili waweze kuwa rasilimali bora yenye tija kwa familia na taifa hivyo shirika la Livingi For Other kujenga Kisima hicho ni hatua kubwa ya kusaidia kundi la watoto wadogo waliokuwa wanakumbwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama.

Nimekwambia hiyo story ipo sawa,rekebisha jina lisomeke Isaack.

Pili , upate maoni ya Mwananchi ambaye alikutana na changamoto ya ukosefu wa kisima aeleze hisia zake juu ya athari

Serikali inatekeleza Program jumuishi ya taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto ambayo moja ya lengo kuu ni usalama wa mtoto mwenye umri kati ya mwaka 0-8.

Mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa ambayo inatekeleza programu hii ili kufikia lengo kuu la taifa la kuhakikisha watoto wenye umri kati ya 0-8 wanakua kulingana na mwongozo wa PJTMMM hivyo kisima hicho ni mkombozi mkubwa kwa watoto hao.
           

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post