WANANCHI wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kupitia kwa Naibu Waziri Nishati na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Judith Kapinga wamemshukuru Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya Umeme, Maji, Barabara, Shule za Sekondari na Msingi pamoja na Afya.
Pongezi hizo zimetolewa leo Septemba 25, 2024 wakati Mh Rais Samia akizindua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Katika Sekta ya Nishati, Mfano wa miradi hiyo ni ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbinga chenye thamani ya shilingi bilioni 3 ambao utatekelezwa katika mradi wa kuboresha gridi ya Taifa Awamu ya Pili.
Aidha kwa upande wa umeme vijijini, katika Jimbo la Nyasa umeme umefika katika Vijiji vyote 84 kwa gharama ya shilingi Bilioni 83.
Social Plugin