AKIMBIA KILOMITA 160 KWENDA KUMUONA MCHUMBA WAKE


Mwanaume mmoja huko San Diego aliyefahamika kwa jina la Aron Greene (26) ametengeneza rekodi ya kipekee na hii ni baada ya kukimbia takribani Miles 100 ambayo ni sawa na kilomita 160 kwa ajili ya kwenda kumuona mchumba wake.

Unaposema kilomita 160 kwa wale ambao wanasafiri mara kwa mara watakuwa mashuhuda juu ya umbali huu, lakini kwa faida ya wengi huu ni umbali kutoka Dar es salaam mpaka Mikese ambayo ni Morogoro.

''Nilikuwa nimesimama kwenye makutano ya barabara kubwa nikasema nadhani naweza kufika kwake kwa kukimbia tu'', alisema Aron Greene ambaye alikuwa anatoka San Diego kuelekea Los Angel alipo mpenzi wake, jambo ambalo lilimchukua takribani saa 32 yaani siku moja na saa 8.

Kama ulihisi huo ndiyo unaweza kuwa ukomo wa Greene basi fahamu kuwa ''Kwa wakati mwingine ningependa kuongeza umbali zaidi na kukimbia hadi John Muir trail'' alisema Greene, hii John Muir trail iko umbali wa miles 211 ambayo ni sawa na kilomita 339, umbali wa Dar es salaam mpaka Tanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post