Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mati super brands LTD David Mulokozi amezindua tawi la mashabiki wa timu ya Soka ya fountain gate FC tawi la Babati mkoani Manyara ikiwa na lengo la kuhamasisha Vijana kupenda michezo na kuiunga mkono timu hiyo iliyohamia Mjini Babati katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa kutoka mkoani Mwanza.
Akizungumza mara baada ya kuzindua tawi hilo Septemba 16, 2024 katika mtaa wa Oster bay amepongeza ubunifu huo wa Vijana walioamua kuwaza jambo hilo ambalo ni kubwa na kwamba Kampuni ya Mati ipo tayari kulisaidia tawi hilo kwa kila namna.
Amesema Mati super brands sio matajiri Sana wala sio masikini Sana kwa sababu wana moyo wa kutoa hivyo kila walichoomba Mashabiki hao katika risala yao wamekipata.
"kupitia Mashabiki hawa itakuwa chachu na hamasa kwa kila Mahali ambapo timu itakwenda nao kufungua matawi kama haya"
"Na Sisi kama wadhamini wakuu tutajitahidi kwa namna Moja ama nyingine kusapoti yale matawi kuyatambua"
Amesema Fountain Gate FC walivyofika kuomba udhamini Mati super brands waliwapokea kwa mikono miwili kwa sababu ni fursa ya kibiashara kwa mji wa Babati na kwa Kampuni kuutangaza bidhaa zao.
Katika risala yao fountain gate Royal fans waliomba kupatiwa Tv kubwa inchi 75 na usafiri kwa ajili ya kusafiri na timu maeneo mbalimbali Nchini.
Hata hivyo uongozi wa Fountain Gate FC umeridhia kufunguliwa kwa tawi hilo ambalo ndo la kwanza nchi nzima na kwamba wapo tayari kutoa Magari matano (Coaster) kusafirisha Mashabiki hao kwenye mechi zao za nje ya Babati.
Nao uongozi wa tawi la Fountain Gate royal fans chini ya mwenyekiti Emmanuel Hondi wamemshukuru David Mulokozi kwa kuwapatia mahitaji hayo pamoja na kuendelea kuiunga mkono Fountain Gate FC kwa kuipa udhamini wa mwaka mmoja.
Social Plugin