Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MATARAJIO MAKUBWA BOMBA LA MAFUTA KUKAMILIKA KWA WAKATI



Na Hamida Kamchalla, TANGA.

MRADI wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) umefikia hatua muhimu katika eneo la Chongoleani, Tanga, ambapo Balozi wa Tanzania nchini Uganda Jenerali Paul Simuli ameelezea umuhimu wa mradi huu kwa uchumi wa nchi hizo mbili.

Jenerali Simuli amesema Bomba hilo ni fursa ya kipekee kwa uchumi wa Tanzania na Uganda na amefanya ukaguzi kuanzia unapoanzia mradi huo hadi Chongoleani ambapo ujenzi unaishia.

Kwa upande wa Uganda amesema eneo la mradi na kwenye visima vya mafuta tayari wameshaweka sample zipatazo sita za kuvutia mafuta kutoka ardhini yalipo, lakini pia wametengeneza sehemu ya kuyahifadhia na kusafisha kidogo kuyaweka katika hali ya usafi.

"Ziara hii nchini nilianzia pale Kagera ambapo ndio tunayapokelea mafuta na shughuli nyingi za Bomba hili zinaanzia pale, nizipongeze serikali zote mbili kwa kazi nzuri za kimaendeleo na kuitisha mikakati ambayo itazifanya nchi hizi kuwa na uchumi stahiki kwa wananchi wake" amesema.

"Vilevile kuwa na mahusiano mazuri ya kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi, lakini pia nimpongeze Rais wetu kwa kuweka nguvu yake yote katika mradi huu wa kimkakati unakamilika na kwa jinsi nilivyokuona unakwenda vizuri" amesisitiza.

Aidha Balozi amebainisha kwamba kulingana na maelezo na utekelezaji na jinsi alivyouona mradi huo matarajio ni makubwa kwamba utakalazeaji utaendelea kuwa wa kiwango kinachokubalika lakini pia utamalizika kwa wakati.

Ameendelea kusema kuwa mradi huo wakati unaanza uliwajali wananchi na kuwapa fidia pesa taslimu na wengine walijengewa nyumba za kisasa, lakini pia ulitoa misaada mbalimbali kwa wananchi kulingana na jinsi mtu alivyoathirika kwenye eneo lake kuanzia ulipoanzia nchini Uganda.

"Kwahyo mradi umewagusa pazuri wale wote walioguswa, lakini umeweza kutoa elimu ya kilimo kwa wananchi wakulima katika maeneo yao kwa jinsi hani wanaweza kutumia eneo dogo kuzalisha, na wafugaji nao hawakuachwa nyuma,

"Walipewa elimu ya ufugaji bora na iujipatia kipato baada ya kuachia maeneo yao kupisha ujenzi huu wa kimkakati, hivyo basi niwaombe Watanzania, isiwe mradi huu tu, bali wowote ule ambao utakuwa wa kimkakati, tuwaige hawa wenzetu waliotoa maeneo yao kupisha maendeleo" amesema.

Amefafanua kwamba katika kambi zote alizopita wananchi wengi wamenufaika kwa kupata ajira ambazo ni za kudumu na za muda ambapo pia aliwataka kutumia fursa hizo kujiendeleza kwa kipato wanachopata kutokana na ajira zao.

"Labda tu niwaombe wale waliyopata zile ajira na kupata kipato, walinde ajira na kutumia vizuri kipato chao ili ajira zitakapofika mwisho, basi kipato kile kiweze kuwasaidia hata kupata mitaji na kuendesha maisha yao endapo watajioanga vizuri" ameonya.

Balozi amesema "ujenzi wa mradi huu ni kielelezo kwamba unafuata zile taratiibu za Kimataifa lakini pia na Taifa letu na nimejionea kila nilipopita, mkakati wao wa kutunza mazingira ni mzuri sana na wanafuata sheria zote, kwahiyo asije akatika mtu mwengine akasema kuna uchafuzi wa mazingira".

Amesema sambamba na hayo mradi unazingatia kutunza na kulinda vyanzo vya maji ambapo baadhi ya maeneo wanasisitiza upandaji wa miti pamoja na kuwapa elimu  wananchi wanaowazunguuka kuacha kuharibu vyanzo hivyo.

"Kwahiyo sioni sababu kubwa sana kama mtu atajitokeza mbele yako wewe Mtanzania kukwambia huu mradi haufai, ni uongo, na wakati mwengine ukute huyo mtu hapendi maendeleo anataka kuturudisha nyuma"  amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com