meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob tayari amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Ni jioni ya leo Alhamisi, Septemba 19, 2024 na anasubiri hakimu aingie mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Jopo la waendesha mashtaka mawakili wa Serikali wakiongozwa Job Mrema pamoja na jopo la mawakili wa Jacob linaloongozwa na Peter Kibatala wapo ndani ya ukumbi wa mahakama sambamba na wanachama wa Chadema.
Boni Yai alikamatwa jana Jumatano, maeneo ya Sinza na Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kumpeleka Kituo cha Polisi cha Osterbay. Kisha usiku wa jana alipelekwa nyumbani kwake Mbezi Msakuzi kwa upekuzi.
Chanzo: Mwanachi digital
Social Plugin