JKT : NAFASI ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA KUJITOLEA HAZIUZWI NI BURE

KAIMU Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Juma Mrai ,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Septemba 25,2024 Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa JKT .
KAIMU Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Juma Mrai ,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Septemba 25,2024 Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa JKT .

Na.Meleka Kulwa-DODOMA

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za kujitolea kwa mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa vijana wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wenye sifa za kujiunga na Jeshi hilo huku watakaopata nafasi hizo wametakiwa kuripoti katika kambi za JKT kuanzia Novemba 1 hadi 3 Mwaka huu.

Akizungumza leo Septemba 25,2024 na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa JKT,Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Kanali Juma Mrai amesema usaili utaanza Oktoba 1, mwaka huu kupitia Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.

“Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana wote watakaopata fursa kuja kujiunga ili kujengewa uzalendo, Umoja wa kitaifa, Ukakamavu, kufundishwa stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao” amesema Brigedia Jenerali Mabena.

Amesema utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anatoka.

Ameongeza kuwa “ Vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti kwenye Makambi ya JKT kuanzia Novemba 1 hadi 3 mwaka huu ,aidha JKT linapenda kuwaarifu Vijana watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajira, wala kuwatafutia ajira kwenye asasi, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali au vyombo vya ulinzi na Usalama” amesema.

Aidha amewaasa wazazi na walezi kujihadhari dhidi ya matapaeli ambao wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kutapeli wananchi kwamba wanaweza kuwasaidia kupata nafasi hizo kwa kutoa pesa ili wajiunge na JKT.

“Mara nyingi nafsi hizo zinapotangazwa wanaibuka matapeli ambao hudai nafasi hizo zinapatikana kwa kutoa fedha,naomba niwaambie nafasi hizo haziuzwi ni bure hivyo kila mmoja aombe sehemu husika zilizotolewa na JKT,”

Sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo vinapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post