Na Frankius Cleophace -Tarime Mara
Jamii wilayani Tarime Mkoani Mara imeomba Mashirika mbalimbali likiwemo shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Kuendelea kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia ili kupunguza vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikitokea hapa nchini.
Hayo yanabainishwa na baadhi ya wananchi katika kijiji cha Surubu kata ya Komaswa wilayani Tarime mkoani Mara wakati wa mjadala wa pamoja uliohusisha kundi la wananaume na wavulana baada ya kuandaliwa na shirika la Jukwaa la Utu wa mtoto CDF.
Agrey Solonyo ni mkazi wa Surubu kata ya Komaswa Wilayani Tarime mkoani Mara akichangia mada zilizoandaliwa alisema kuwa elimu indelee kutolewa kwa lengo la kubadili mitazamo hasi iliyojengwa kwenye jamii ili kuondokana na vitendo vya Ukatili hususani kwa watoto wadogo.
Ukiangalia matukio mengi yamekuwa yakitoke hapa Nchini yakiwemo ya Ubakaji, Ulawiti Vipigo na mara nyingi yanawakabili watoto wadogo ambao hawana uwezo wa kupaza sauti hivyo sasa ni jukumu la serikali pamoja na mashiriki kuendelea kupaza suti.
“Ukatili bado upo kwa mfano vipigo kwa watoto wadogo ili kumaliza hivi vitendo elimu iendelee kutolewa kwa makundi yote kuanzia shule za msingi hadi sekondari pia elimu iwe endelevu”alisemo Solonyo.
Kwa upande wake Hassan Bijampole aliongeza kuwa kuna haja kubwa ya kuendelea kujengea uwezo mkubwa viongozi wa dini ili nao sasa waeneza elimu hiyo kwenye jamii kwa lengo la kupunguza vitendo vya Ukatili wa kijinsia.
“Viongozi wa dini wanahaminika kwenye jamii sasa serikali pamoja na mashirika waweke nguvu kubwa kwa viongozi hao wa dini ili elimu iendelee kutolewa kwa lenmgo la kulinda kizazi chetu misingi bora ya utu inapaswa kulindwa alisema Bijampola”.
Hassan aliongeza kuwa jamii imeona ni kawaida kutendeka kwa ukatili huo sasa nguvu ya pamoja iunganishwe kwa lengo la kuhakikisha wanaotenda ukatili kwa watoto waweze kufikishwa sehemu huska nakupatiwa adhabu kali na kwa wakati kwani wengi wamekuwa wakiachiwa nakurudi kutisha wale waliotoa taarifa za ukatili huo.
Naye Raphael Wambura aliongeza kuwa kuna haja kubwa ya kutungwa kwa sheria ndogondogo kuanzia ngazi ya familia vijiji, kata wilaya hadi hadi taifa ili kuwatia nguvuni wale wote wanaendeleza ukatili wa kijinsia.
Alice Mtuga ni mratibu wa mtandao wa Ushiriki wa wanaume na wavulana Tanzania kutoka Shirika la Jukwaa la utu wa Mtoto CDF anasema kuwa wameamua kuusisha kundi la wanaume kwa sababu limesaulika pia lina sauti kwenye familia hivyo elimu watakayopatiwa itaaidia kuelimisha jamii ili kupunguza vitendo vya Ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kulinda kundi la watoto.
“Watoto n Tunu ya Taifa motto anapaswa kulindwa akiwa tumboni na wakati wa kuzaliwa sasa kundi la wanaume limesaulika hivyo kupitia elimu hii tunayoitoa nadhani watoto watakuwa salama zaidi”, alisema Alice.
Aidha Lucy John ambaye ni mkurugenzi wa shirika la Wadada Solutions on Gender Based Violence anasema kuwa serikali kwa kushirikiana na mashiriki ione sasa njia bora ya kuweza mazingira rafiki kwa wale wote wanaotoa taarifa za ukatili ili wasiweze kuzuliwa kwenye jamii zinazowazunguka.
“Tumeona hoja imeibuka kwenye huu mjadala kuwa wale wanaotoa taarifa za ukatili wanatishiwa maisha yao sasa ni jukumu le serikali kwa kushirikiana na Mashiriki kuhakikisha wanalinda watu hao ili taarifa za ukatili ziendelee kutolewa kwenye jamii kwa lengo kufanyia kazi ukatili huo” alisema Lucy.
Uandaaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya MMMAM umezingatia ushirikishwaji wa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali, wadau wa maendeleo, na mashirika yasiyo ya kiserikali hivyo sasa wakiendeleza umoja wao watoto kuanzia miaka 0-8 wakilindwa na kujengewa misingi bora tutakuwa na Taifa lenye watoto salama ambao hawajakumbwa na Ukatili wa aina yeyote