MATI SUPER BRANDS YASHIRIKI MANYARA DAFTARI DAY JOGGING

 



Na Mwandishi Wetu ,Manyara.


Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited imeshiriki na kudhamini Matembezi maalumu ya kuhamasisha Wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura yanayofahamika kama "Manyara Daftari Day " ambapo Mamia ya wakazi wa mkoa wa Manyara wameshiriki matembezi hayo yaliyofanyika katika viwanja ya Tanzanite Kwaraa Stadium.

Akizungumza mara baada ya kushiriki matembezi ya Kilomita 4.4 yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga ,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa wamedhamini matembezi hayo ili kuhamasisha Wananchi kushiriki kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kuwachagua viongozi wanaowataka.

Mulokozi amesema kuwa kampuni hiyo ni sehemu ya Jamii na imekuwa ikiunga mkono shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo matembezi hayo ambapo amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kugombea nafasi mbali mbali ili kupata viongozi bora watakaoleta maendeleo kuanzia ngazi ya mtaa,vijiji,kata,jimbo na Taifa.

"Tumeanza kuhamasisha vijana kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapira kura hata kwenye viwanda vyetu kuhakikisha kuwa wanajiandikisha na ikiwapendeza wanaweza kuweka kituo maalumu karibu na kiwanda chetu ili vijana wengi waweze kujiandikisha",ameeleza Mulokozi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika zoezi la maboresho ya daftari la wapiga kura litakaloanza Septemba 4 hadi 10 mwaka huu.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post