MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu,akizungumza wakati alipokuwa mgeni maalum katika hafla ya uzinduzi iliyofanyikia Kanisa la KKKT lililopo Ikungi.
......
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameshiriki Uzinduzi wa Jimbo la Ikungi KKKT na kuchangia vifaa vya ofisini vyenye thamani ya Shilingi Milioni 11.
Vifaa hivyo ni pamoja na kompyuta,printa,Photocopy na samani za ofisi ikiwa ni maombi yaliyokuwemo kwenye risala iliyosomwa na Mkuu wa Jimbo Jipya la Ikungi Mch.Sara Msengi.
Aidha,amewakumbusha kuwa Mwaka huu 2024 ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali Za Mitaa,vijiji na Vitongoji hivyo kupitia jukwaa lao wawahimizw wananchi kujitokeza kuchagua viongozi wanaona wanawafaa katika kuleta maendeleo.
Mtaturu ametoa salamu hizo ,alipoalikwa kama mgeni maalum katika hafla ya uzinduzi iliyofanyikia Kanisa la KKKT lililopo Ikungi.
"Nifikishe salamu za Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenu kwa kuendelea kushirikiana na serikali kutoa huduma za kijamii kwenye sekta za Elimu na Afya,niwaombe muendelee na kazi ya kuliombea Taifa na kuwalea waumini kiroho ili waendelee kulina tunu ya amani,
"Nikupongeze Askofu wa Dayosisi ya Kati Dkt Syprian Yohana Hillint kwa kuendelea kuliongoza kanisa vizuri toka umechaguliwa na kusimikwa,hongera sana,"amepongeza
Akizungumzia uchaguzi unaokuja amewaomba waumini muda ukifika kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Uchaguzi wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la wapigakura ili wapate sifa ya kupiga kura.
Akizungumza kwenye Ibada maalum ya uzinduzi wa jimbo la KKKT Ikungi Askofu Hilint amesema hilo ni Azimio la Halmashauri Kuu ya Dayosisi.
Amewahimiza waumini kushiriki kulijenga Jimbo jipya.
"Tunaendelea kuwaombea na kuwapatia msaada ili wafikiwe mtarajio yao,"amesema.
Social Plugin