MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngamiani Kati wakati wa mkutano wake wa hadhara katika eneo hilo
Na Oscar Assenga,TANGA
MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu
kwa uwekezaji mkubwa katika Bandari ya Tanga ambao matunda yake yameanza
kuonekana kwa kuiwezesha kupokea shehena kubwa ikiwemo za magari.
Ummy
aliyasema hayo leo wakati wa mkutano wake wa hadhara uliofanyika kata ya
Ngamiani Kati Jijini Tanga ambapo alisema hilo ni jambo kubwa sana
ambalo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa wananchi .
Alisema
kwamba uwekezaji huo wa zaidi ya Bilioni 400 uliofanywa na Serikali
umekuwa ni chachu kubwa ya kufungua fursa za kiuchumi katika mkoa
waTanga na sasa hata Jiji hilo limeanza kubadilika.
Alisema
kwamba kutokana na uwekezaji huo utasaidia kuwezesha uchumi wa mkoa wa
Tanga kukua kutokana na shehena za mizigo zinapokuwazikishushwa kwenye
Bandari hiyo wananchi watanufaika.
"Uwekezaji
huu kwetu sisi watu wa Tanga ni mkubwa wenye manufaa makubwa kwani
utatusaidia kuweza kurudisha enzi zetu za miaka ya nyuma kukua kiuchumi
na hii italeta manufaa kwetu sote hivyo niwatake wana Tanga kuchangamkia
fursa hii"Alisema
Aidha
alisema kwamba awali kabla ya uwekezaji huo walikuwa wakikosa fursa za
kuona meli kubwa zikitia nanga gatini lakini kwa sasa imekuwa ni rahisi
kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali.
Alisema
jambo hilo limesaidia kuwarudisha wafanyabiashara ambao awali walikuwa
wakitumia Bandari hiyo na hivyo kupelekea uwepo wa mzunguko wa
kibiashara kwenye Jiji hilo.
"Ndugu
zangu wakati natafuta kura mwaka 2020 mkoani kwetu hakukuwahi kuwa na
meli kubwa tena ambazo zinashusha magari na kutia nanga gatini lakini
kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa Serikali kupitia mimi Mbunge wenu
zimeleta matunda na hivyo Rais Dkt Samia Suluhu kutuletea fedha ambazo
zimewezesha maboresho makubwa yaliyowezesha meli kubwa kutia
nanga"Alisema
Hata hivyo
aliwataka wakazi wa Jimbo hilo kuchangamkia fursa ya maboresho
yaliyofanywa kwa kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali ya
kiuchumi,ujasiriamali na kilimo kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi
zinazotokana na uwekezaji huo.
Social Plugin