MKURUGENZI M TOURS ATEMBELEA MAKUYUNI WILDLIFE PARK



Na Mwandishi Maalum, TAWA

Mkurugenzi wa Kampuni maarufu ya utalii inayofahamika kama M Tours, Bi. Elvera Verhagen akiwa ameambatana na babu yake Bw. Van Denzel kutoka Uholanzi tarehe 6/9/ 2024, walitembelea eneo la Makuyuni Wildlife Park lililopo wilayani Monduli jijini Arusha kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo na kupata fursa ya kufahamu namna wanavyoweza kufanya biashara ya utalii katika eneo hili hasa Utalii wa Kuendesha Baiskeli.
Uwepo wa miundombinu wezeshi ya barabara, wingi wa wanyamapori na mandhari ya kuvutia huifanya Makuyuni Wildlife Park kuwa chaguo bora kwa mtalii yeyote wa ndani na nje ya Tanzania.

Shughuli nyingine za kitalii zinazoweza kufanyika katika eneo hilo ambalo ni makazi ya wanyamapori wakubwa wanne (Big Four) ambao ni Nyati, Simba, Tembo, ni pamoja na kupanda mlima (Hiking), utalii wa kutembea kwa miguu (Walking Safari),Utalii wa kuona ndege, jua likichomoza na kuzama, utalii wa Utamaduni (jamii ya kabila la wamasai inayozunguka eneo hili).

Makuyuni Wildlife Park ni eneo lililo chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA ambalo Mamlaka hiyo ilikabidhiwa na Serikali hivi karibuni ili iweze kulisimamia na kuliendeleza ikiwa na pamoja na kulinda rasilimali wanyamapori zilizopo katika eneo husika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post