POLISI ,SUNGUSUNGU SHINYANGA WAKUTANA NA JESHI LA SUNGUSUNGU MANYADA ,WAHIMIZA AMANI NA MSHIKAMANO

Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha akishirikiana na Viongozi wa jeshi la Sungusungu mkoa wa Shinyanga wamekutana na vikundi vya ulinzi shirikishi maarufu sungusungu pamoja na wananchi wa kijiji cha Manyada Kata ya Usanda iliyopo Tarafa ya Samuye Wilaya na Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutoa elimu ya Polisi Jamii.

Elimu hiyo imetolewa Septemba 06, 2024 ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi itakayofanyika Septemba 17, 2024 inayojulikana kama Siku ya Jeshi la Polisi Tanzania.

ACP Tesha amewataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na vikundi vya ulinzi shirikishi ili kufichua vitendo vya uhalifu na wahalifu katika kata na Wilaya kwa ujumla.

Awali Kamanda wa jeshi la Sungusungu mkoa wa Shinyanga John Kadama amesema kuwa lengo la kuandaa mkutano huo ni kutaka kusikiliza na kutatua migogoro na kero zinazo wakabili wananchi wa kijiji cha Manyada pamoja na sungusungu wakata hiyo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwasimamiza baadhi ya viongozi wa sungusungu katika kata hiyo kwa kile kinachotajwa kuwa wao wamekuwa ni kichocheo cha migogoro baina ya wananchi na jeshi hilo.

Naye Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Shinyanga Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Oswald Nyorobi amewashukuru wananchi wa Kijiji cha Manyada na kata ya Usanda kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha usalama unaendelea kuimarika.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Usanda Mhe. Foresti Nkole kwa niaba ya wananchi ameshukuru ujio wa kamati hiyo ya Polisi Jamii Mkoa kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi na kuahidi kuendelea kulinda amani katika Kata hiyo. 
Viongozi wa Sungusungu mkoa na Jeshi la polisi wakielekea kwenye mkutano wa Sungusungu Kijiji cha Manyada.
Viongozi wa Sungusungu mkoa na Jeshi la polisi wakielekea kwenye mkutano wa Sungusungu Kijiji cha Manyada.
Kiongozi wa Jeshi la Sungusungu mkoa wa Shinyanga John Kadama akizungumza na Sungusungu wa kijiji cha Manyada.
Viongozi wa Sungusungu mkoa na Jeshi la polisi wakielekea kwenye mkutano wa Sungusungu Kijiji cha Manyada.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post