MZEE WA UBWABWA ATETEA NAFASI YAKE YA UENYEKITI CHAUMMA


Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Hashimu Rungwe amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa chama hicho taifa kura 118 kati 120 katika uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar Essalam.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Mohamed Masoud amesema nafasi ya mwenyekiti mgombea alie jitokeza ni mmoja na amepigiwa kura ya ndiyo au hapana

Hashimu Rungwe ametetea nafasi hiyo kwa muhura wa tatu tangu chama hicho kianzishwe.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine Rungwe ameshukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kuendelea kumuamini na kuwa atandelea kuisimamia sera yake ya Ubwabwa mashuleni na hosptalini huku pia akisisitiza kuwa mpango wa chama kupeleka bahari Dodoma ukiwa palepale.

Naibu msajili kutoka ofisi ya msajili wa Vyama vya Siasa Sist Nyahoza amekipongeza chama hicho kwa kufanya siasa za ustarabu na kusimamia tunu za taifa ikiwemo amani.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post