Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ( Mb) ametoa wito kwa wafanyabiashara wote nchini kuchangia pato la Taifa kwa kulipa kodi kwa hiari.
Mhe. Kigahe ameyasema hayo wakati akijibu hoja za wafanyabiashara wa Ngara katika Mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari ya Ngara.
Katika kiko hicho, Wafanyabiashara hao wamewasilisha hoja mbalimbali ikiwemo utitiri wa Biashara za magendo na zisizo fuata utaratibu zinazoingia nchini Tanzania kutoka nchi jiarani na kuuzwa nchini kwa bei nafuu tofauti na bidhaa za hapa nchini zinalipiwa kodi na kuingizwa kwa njia rasmi.
"Ndugu zangu niwaombe sana sisi kama Serikali tumesikikiza hoja zenu, zile zinazowezekana tutazifanyia kazi, pia nanyi mtimize wajibu wenu kwa kulipa kodi. Mnapolipa kodi bila shuruti mnaiongezea Serikali pato ambalo litasaidia kuteleleza miradi ya Maendeleo na kuinua uchumi wa nchi "Amesema Kigahe.
Ameongeza kwa kusema kuwa licha ya kupoteza mapato ya Taifa pia wananchi wanapata madhara ya kiafya kwa kula vyakula ambavyo vinaingizwa hapa nchini kinyemela bila kuwa na ubora wa TBS
Aidha, Mbunge wa jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba Ruhoro ameishukuru Wizara ya Viwanda na Biasha kwa kufika katika Wilaya ya Ngara kujibu na kutolea ufafanuzi mzuri juu ya hoja za Wafanyabiashara.
"...Wananchi wa Ngara wanapata changamoto z Kibiashara kupitia Mipaka ya Kabanga na Rusumo. Mipaka hii ni mikubwa na Biashara za magendo zinaadhiri biashara za wananchi wetu". Amesema Mhe. Ndaisaba Ruhoro.
Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wilaya ya Ngara Bw. Chrispine Kamugisha amemweleza Naibu waziri wa Viwanda na Biashara kuwa changamoto za mipakani ni endelevu kwasababu ya mifumo inabadilika mara kwa mara ambapo hupelekea wafanyabiashara kufilisika.
"Wafanyabiashara wanapofilisika huwa wanakuja wengine wapya kufanya Biashara hivyo tunaomba Wizara kuwa na zoezi endelevu la kutoe Elimu kwa wafanya Biashara wapya `` Amesema Kamugisha.
Kwa upande wake Hafidhi Abdalah ambae ni Mfanyabiashara wa Wilaya ya Ngara amewasilisha hoja zake ikiwemo changamoto ya mikopo ya benki pale wanapopewa mkopo wanadaiwa baada ya mwezi mmoja kurudisha marejesho wakati ambao wanakuwa hawajaanza kufanya Biashara.
Bernadeta Kanyankole Mfanyabiashara wa Ngara amelalamikia uwepo wa utitiri wa kodi kwenye biashara moja huku akiomba kuwa na mifumo inayosomana ili mfanyabiashara anapolipa kodi au ushuru wowote mifumo isomane ili kuondoa kero ya maafisa wa TRA kuwatembelea mara kwa mara kwenye Biashara zao kudai Kodi.
Social Plugin