RAIS SAMIA ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA VITA VYA MAJIMAJI, SONGEA MKOANI RUVUMA


Matukio mbalimbali wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Songea mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Songea mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi wakati akielekea Songea mjini wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la pamoja la Mashujaa wa Vita vya Majimaji walionyongwa na Wajerumani tarehe 27/02/1906 wakati wa Vita hivyo mjini Songea. Rais Dkt. Samia ameanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ambapo atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoka kwenye moja ya nyumba ya utamaduni wa asili ya Wangoni iliyopo katika Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Songea mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post