Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA: -HUDUMA ZIFANANE NA UZURI WA JENGO

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga mkoani Ruvuma tarehe 25 Septemba, 2024.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia amesema: 

"Niipongeza sana halmashauri ya Mbinga kwa kuamilisha ujunzi huu wa jingo hili. Ni jingo zuri nimeingia ndani kuangalia ujenzi unaridhisha sana na ni jingo lenye nafasi za kutosha, kwa hiyo niwashukuru sana. Ndugu zangu wa Mbinga kukamilika kwa jingo hili ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ambayo imetutaka tujenge majengo ya halmashauri ili kutoa nafasi ya kuhudumia vizuri wananchi lakini pia kukuza utawala bora. Kwamba haki za wananchi zinashughulikiwa haraka iwezekanavyo na zote ni pahali pamoja. Aidha kwa watumishi pia kuhakikisha huduma zinazotolewa humu ndani ziendane na uzri wa jengo hili".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com