TANZANIA, CHINA KUSHIRIKIANA USIMAMIZI WA SHERIA NA USALAMA WA UMMA









Na Mwandishi Maalum, CHINA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania Mhe. Daniel Sillo amefanya kikao cha ushirikiano ( Bilateral meeting) na Mhe. Chen Siyuan, Naibu Waziri wa Usalama wa Umma wa China na kujadiliana naye maeneo ya ushirikiano wa usimamizi wa sheria na usalama wa umma kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Usalama wa Umma wa China.
Katika kikao hicho kilichofanyika leo Septemba 7, 2024 katika Jiji la Beijing Nchini China, viongozi hao wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika kupambana na uhalifu wa kupanga na kuvuka mipaka kama vile ugaidi,dawa za kulevya, usafirishaji harama wa binadamu,makosa dhidi ya fedha ,makosa dhidi ya nyara za Serikali na uhalifu kwa njia ya Mtandao.

Aidha, wamekubaliana kuongeza matumizi ya teknolojia ya kisasa, kufanya utafiti wa pamoja kubadilisha ujuzi na uzoefu pamoja na kutoa mafunzo ya kisasa kwa maafisa wa Jeshi la Polisi ikiwemo pia kuimarisha ulinzi kwenye miradı ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya China na Tanzania.

Katika tukio lingine Naibu Waziri na ujumbe wake aliishiriki Kikao cha Kwanza cha Ngazi ya Mawaziri na kushuhudia kusainiwa Hati ya Makubaliano (MoU) ya Ushirikiano wa Usimamizi wa Sheria na Usalama Umma kati ya China na Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika ( EAPCCO).

Jumla ya Mawaziri na Wawakikishi kutoka nchi 14 zilishiriki mkutano huo uliongozwa na mwenyeki Mhe. Wang Xiaohong na Mwenyekiti mwenza Mhe. Davidi Nitetse ambaye ndiye Mwenyekiti wa Mawaziri wenye dhamana ya kusimamia Majeshi ya Polisi katika Ukanda wa Mashariki ya Afrika.

Ujumbe huo kesho Septemba 9 na Septemba 10, 2024 utashiriki Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano wa Usimamizi wa Sheria na Usalama duniani katika mji wa Lianyungang nchini China.

Mhe. Daniel Sillo ameongozana na Dkt. Maduhu Kazi, Naibu Katibu Mkuu na Kamishna wa Polisi Faustine Shilogile.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post