SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendela kutoa elimu ya ubora wa bidhaa katika Maonesho ya saba ya Mifuko na Programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yaliyofanyika katika viwanja vya Bombadier mkoani Singida.
Akizungumza katika Maonesho hayo ambayo yameanza Septemba 8,2024 na kumalizika Septemba 14, 2024, Afisa mtoa elimu, Sileja Lushibika amesema TBS imeshiriki na kutoa elimu kwa wajasririamali pamoja na wageni waliofika katika banda la Tbs juu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na umuhimu wa kuwa na alama ya ubora ya Tbs katika bidhaa. Afisa mtoa elimu ni Sileja Lushibika.
Ushiriki wa TBS katika maonesho haya ulionyesha dhamira yake ya kuunga mkono juhudi za kiuchumi za wananchi na kutoa mchango wa kipekee katika maendeleo ya sekta ya viwanda na biashara nchini Tanzania.
Social Plugin