TEA & TOTALENERGIES MARKETING LTD WAKABIDHI MADWATI 130 WILAYANI KIBITI


Kampuni ya TotalEnergies Marketing Ltd kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamekabidhi madawati 130 katika shule ya Msingi Jaribuni Mpakani na Shule ya Msingi ya Kitundu za Wilayani Kibiti Mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ushirikiano baina yao katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

Hafla ya kukabidhi madawati hayo iliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani tarehe 24 Septemba 2024.

Akizungumza katika hafla hiyo Kanali Kolombo ameahidi kuwa madawati hayo yatatunzwa vizuri kwa manufaa ya wanafunzi wa shule hiyo na kuongeza kuwa Wilaya ya Kibiti imekuwa ikinufaika na miradi kadhaa ya TEA ukiwemo wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Kitundu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd Bi. Getrude Mpangile amesema madawati hayo 130 ni sehemu ya madawati 200 yenye thamani ya Sh. Milioni 25.9 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa shule tatu za Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.

Kufuatia msaada huyo Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani imepata madawati 65, Shule ya Msingi Kitundu madawati 65 na Shule ya Msingi Makuburi ya Jijini Dar es Salaam imepata madawati 70.

Bi. Ambangile ameeleza matumaini yake kwamba msaada huo utasaidia kuweka hamasa kwa wanafunzi kujifunza kwa bidii na hivyo kuchangia kukuza ufanisi na ufaulu wa shule zilizonufaika na madawati hayo.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, CPA Mwanahamisi Chambega amekumbusha shule zilizonufaika na msaada huo wa madawati kuyatunza vyema.

“Miongoni mwa majukumu ya TEA ni kutafuta raslimali fedha kutoka kwa wadau mbali mbali na kuzigawa katika taasisi za elimu ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia hivyo tunawakumbusha kutunza vifaa hivo”. Amesema CPA Chambega.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo (Kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, CPA. Mwanahamisi Chambega katika hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.

Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total Energies Marketing Tanzania Ltd Bi. Getrude Mpangile (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA CPA. Mwanahamisi Chambega katika hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani wakifuatilia hafla ya kukabidhiwa madawati 

Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd Bi. Getrude Mpangile akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitundu ambayo pia imenufaika na msaada wa madawati 

Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Bi. Zakayo Mtenduka (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, CPA. Mwanahamisi Chambega katika hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Jaribu Mpakani

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo katika picha ya pamoja na viongozi waliohudhuria hafla ya kukabidhi madawati katika Shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TEA, CPA. Mwanahamisi Chambega akitoa salaam katika hafla ya kukabidhi madawati katika shule ya Msingi Jaribuni Mpakani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post