Na Oscar Assenga,TANGA
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) imepongezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge Maji na Mazingira kwa utunzaji mzuri wa mazingira katika maeneo yanayozunguka kwenye vyanzo vya maji ikiwemo Bwala la Mabayani Jijini Tanga.
Kamati hiyo imekagua chanzo cha maji cha Mabayani ambacho ni chanzo kikubwa kunacho hudumia jiji la Tanga na mtambo wa kutibu na kuzalisha maji wa Mowe
Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jackson Kiswaga wakati wa ziara ya siku moja ya kutembelea vyanzo vya maji ambapo wakiwa kwenye eneo hilo walieleza kufurahishwa na utunzaji wa mazingira yanayozunguka vyanzo vya maji
Mwenyekiti huyo alisema lengo la ziara hiyo ni kuona namna fedha zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika kutekeleza miradi ya maji na kuelezwa kuridhishwa kwa namna utekelezaji wake unavyofanyika.
“Tumefurahishwa na utekelezaji wa miradi hivyo tuhakikisha wananchi tunawapa maji na utekelezaji wa mradi wa hatifungani uanze haraka ili kutimiza azma ya Rais Dkt Samia Suluhu Kumtua mama ndoo kichwani ” Alisema Kiswaga
“Lakini kubwa sha Tanga Uwasa kwa ubunifu na uuzaji wa hatifungani ya kijani ambayo imeweze upatikanaji wa fedha kiasi cha sh.Bilioni 53.12 ambazoo zinakwenda kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya Tanga ,Mkinga,Muheza na Pangani”Alisema
Hata hivyo waliipongeza Wizara ya Maji na Mammlaka yAmeipongeza Wizara ya Maji na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuwapeleka huduma ya maji wananchi ili kuondosha tatizo la uhaba wa maji katika jiji la Tanga.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Waziri wa Maji Jumaa Aweso alisema baada ya kupatikana kwa fedha kiasi cha Bilioni 54 kutokana na mradi wa maji Hatifungani tayari wameshampata mkandarasi kwa ajili ya kuboresha mradi wa maji wa tanga Uwasa na wananchi zaidi ya laki sita watanufaika.
Waziri Aweso alisema mpaka sasa wakandarasi tayari wamekwisha kupatikana ambao ni China Railway Co Limited na STC Construction Co Limited huku akieleza hivi sasa ni muda wa kuanza rasmi utekelezaji wa mradi huo ambao umelenga kuongeza uzalishaji wa maji kutoka Lita Milioni 45 hadi Milioni 60 na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi Octoba 2025.
Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian alisema hali ya upatikanaji wa maji kimkoa ambapo alisema maeneo mengi yanapata maji kwa asilimia 59 mpaka 60 kwenye wilaya nane za mkoa huo na juhudi za kuhakikisha wanapata maji zinaendelea.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema ni matarajio yao baada ya mradi huo kukamilika Tanga Jiji watapata maji kwa zaidi ya asilimia 98 na kuwafikia wananchi zaidi ya laki sita.
Wilaya ambazo zitanufaika na mradi huo wa maji ni Jiji la Tanga, Muheza, Pangani na Mkinga
Social Plugin