Mahakama ya Hakimu Mkazi (kituo Jumuishi Cha utoaji haki) Dodoma kimewahukumu Kifungo Cha maisha Jela na faini ya shilingi milioni 1 Kwa Washtakiwa wa shauri la Ubakaji na ulawiti wannee ambao ni Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) MT 140105 Clinton Damas maarufu Nyundo, Amini Lema maarufu Kindamba, Nickson Jackson maarufu Machuche na Askari wa Jeshi la Magereza C 1693 Praygod Mushi.
Akizungumza nje ya Jengo la Mahakama hiyo Mkurugenzi msaidi wa ofisi ya Taifa ya mashtaka Lenatus Mkude amesema kuwa washtakiwa hao wamekuwa na hatia hiyo ya kufungwa Kifungo Cha maisha na faini ya shilingi milioni moja kila mmoja ambapo fedha hizo zitaelekezwa Kwa muhanga wa tukio Hilo la ubakaji binti wa Yombo Dovya.
Mkude amesema zaidi ya mashahidi 18 upande wa mashtaka wametoa ushahidi na vielelezo 12 vimetolewa kwenye shauri Hilo ambapo Leo Sept 30,2024 maamuzi yamefikiwa na mahakama hiyo Kwa kuwapa adhabu ya Kifungo cha miaka 30 Jela na faini ya shilingi milioni moja.
Shauri Hilo ambalo lilikuwa likisikilizwa kwenye mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi(kituo Jumuishi Cha utoaji) na hakimu Zabibu Mpangule.