Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WADAU WAZUNGUMZIA MAANDAMANO YA CHADEMA, "RAIS SAMIA ANAIFAHAMU DEMOKRASIA"

 

DAR-Wananchi mbalimbali wamelaani vikali kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kudai wanafanya maandamano, kwani kitendo hicho kitapelekea kuleta machafuko nchini.
Septemba 11, 2024, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alitangaza Septemba 23,2024 wanafanya maandamano jijini Dar es Salaam.

Pia,wamewataka wananchi wenzao kuwa makini katika kushiriki kwenye maandamano ambayo CHADEMA wamekuwa wakiyafanya, kwani wamekuwa wakiyafanya kwa manufaa yao binafsi.

Aidha,wamelaani kitendo cha chama hicho kuwadhalilisha wanawake kupitia kauli yao ya kumsema mwanamke ambaye hajapata mtoto ‘Mgumba’ kwani kitendo hicho hakiendani na maadili katika jamii kwa ujumla.

Wananchi hao wamepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha uhuru wa vyama vya siasa unakuwepo nchini hasa kwa kuruhusu mikutano ya hadhara na maandano huru nchini.

RAIS SAMIA AMEHAKIKISHA UHURU WA VYAMA VYA SIASA UNAKUWEPO

“Mama Samia alikuwa yupo sahihi, alikaa na kuangalia kwamba uhuru wa vyama vya siasa haupo, Mama Samia akaamua kwamba sasa uhuru uwepo na vyama vya siasa vipo, isipokuwa baadhi ya vyama vipo, lakini haviendi vizuri kama vile alivyotarajia yeye.

"Mama alikuwa na misimamo mizuri ya kuhakikisha kwamba siasa iende kwa taratibu na mikutano ifanyike hii ni sehemu moja ya uhuru wa vyama vya siasa.

“Niwasihi vijana huu siyo wakati wa kutumika unapoambiwa leo twende kwenye maandamano kwanza unatakiwa ujitahmini linalotokea nani atakayeumia.”

VIJANA WASISHAWISHIKE

“Suala la uhuru,Mama anaenda vizuri, hawa wanaofanya hivi kila kunapokaribia uchaguzi ili kutaka kumchafua lazima wadhibitiwe kwa sababu wanataka kuhatarisha amani wakati nchi yetu haina kitu kama hicho.

"Na ina amani kubwa kabisa kuliko nchi zingine, vijana wasishawishike kwani wakati wao wanawashawishi watu, wao wanakaa nyuma hivyo wasishawishike,” amesema Rajab Salehe mkazi wa Dar es Salaam.

WASITUCHAFULIE AMANI

“Kwa nini wao kila mwaka? Serikali iliangalie suala hili, tunataka tufanye uchaguzi wa raha kabisa.

"Mwanzo walisema wanataka wafanye mikutano Rais Samia akawafungulia, fursa wamepata za kuandamana na kufanya mikutano, wafanye mikutano bali wasitichafulie amani,"amesema Fakih Abdllah mkazi wa Dar es Salaam.

KWA SASA SINA IMANI NA CHADEMA

“CHADEMA ni chama cha siasa, hapa hawajachukua madaraka, wameanza kututukana sisi wanawake, je wakija kuchukua madaraka itakuaje?.

"Kwa sisi watoto wa kike sura zetu tutaficha wapi? Hili suala wanawake wenzangu siyo suala la kulifumbia macho kabisa.

"Ikiwezekana ichukuliwe hatua, Chama cha CHADEMA kwa sasa sina imani nacho kabisa na kwa vitendo wanavyovifanya imani imenipotea kabisa."

SITAWEZA KUKIFUATILIA CHAMA CHA CHADEMA KWA SABABU YA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE

“Ugumba siyo kwamba binadamu anapanga, bali anayepanga ni Mwenyezi Mungu na mtu ukipata mtoto ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu.

"Kwa jinsi walivyomzungumzia Lady Jaydee kwamba ni mgumba, sitaweza tena kukifuatilia hiko chama cha CHADEMA, kwa sababu kama wamemdhalilisha mwanamke mwenzetu ina maana hata wakichukua uongozi bado wataendelea kudhalilisha wanawake zaidi.”

WALICHOKIFANYA CHADEMA KWA KUDHALILISHA WANAWAKE HAKIFAI KATIKA JAMII

“Nikiwa kama Mama kwa kitendo walichojifanya kwa kumtukana ina maana hawajamtukana mama bali wamewatukana wamama wote, ni kitu ambacho ni cha kuuzunisha sana na hakiko sahihi kwa jamii.”

MAANDAMANO YALIYOANDALIWA NA CHADEMA HAYANA TIJA KWA TAIFA

“Maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA hayana tija na wala hayana faida kwa Taifa letu kwa sababu uhuru alioutoa mama ni mkubwa sana wa kufanya mikutano na mambo mbalimbali ya msingi, vijana na wananchi kwa ujumla tuwe makini na haya mambo ambayo yanafanywa kwa manufaa ya mtu binafsi.”

RAIS SAMIA ANAIFAHAMU DEMOKRASIA

“Rais Samia anaifahamu demokrasia, leo hii anaweza kukaa na vyama vya upinzani hususani na CHADEMA na kujadiliana nao, amefungua milango na mikutano inafanyika, baadhi yao wanatumia mikutano hii kueleza sera zao na baadhi ya vyama hawatekelezi yale yanayotakiwa,” anasema Suleimani Kasmir mkazi wa Dar es Salaam.

WANANCHI TUSIPOJITAMBUA, CHADEMA WATATULETEA MACHAFUKO

“Katika kitu ambacho tunajivunia watanzania ni amani tuliyonayo, hiki ni kitu kizuri cha kujivunia.

"Lakini, kuna watu wanakuja kwa sababu zao za kinjaa wanataka kufanya amani ibomoke, mama kwa busara na upendo wake kwa wananchi amefanya haki sawa kwa kila mtu wao wanakuja kumtukana.

"Chama cha CHADEMA katika nchi hii tusipojitambua sisi wananchi watatulitea sana machafuko, muogope sana mtu anayetumia mabavu kutaka utawala, huyo mtu ni hatari na ni adui wa Taifa,”amesema Ngayoma mkazi wa Dar es Salaam. TAZAMA VIDEO HAPA CHINI;

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com