SERIKALI imeshauriwa kuongeza Bajeti kwenye mapambano ya magonjwa yasiyoambukiza ili kupunguza magonjwa hayo kwa sasa kwenye jamii.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mshauri wa masuala ya Kijinsia na ujumuishi wa Makundi maalum, Mary kalavo,wakati uchambuzi wa kijinsia kwenye sekta ya Afya ya mwaka 2024-2025 ili kujadili na wadau mbalimbali kuhusu nini kifanyike.
Kilavo,amesema ni wakati wa serikali iongeze fedha kwa ajili ya mapambano ya magonjwa yasiyoyakuambukizwa ikiwemo Kisukari,presha na Figo ambayo yameonekana kuongezeka.
"Licha ya kuwepo na Taasisi za Serikali zinasimamia matumizi ya Vyakula na vinywaji lakini bado kumekuwa na matumizi ya pombe zisizo na sifa na kupelekea serikali kupata mzigo wa kumuhudumia mgonjwa wa Figo."Amesema Kalavo.
Amesema Serikali ikiongeza fedha itasaidia kupunguza gharama kwa serikali katika kuwahudumia watu wenye magonjwa hayo.
Hata hivyo, Kalavo,amewasihimiza watanzania kupenda tabia ya kufanya mazoezi ili kuweza kupambana na magonjwa hayo.
Kwa upande wake Mtafiti kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Aikande Kileo,amesema wamekutana hapo kwa lengo kukagua na kuthibitisha matokeo ya uchambuzi wa Bajeti ya mwaka 2024-2025,huku wakitazamia suala la usawa wa kijinsia limetazamwa kwenye Bajeti hiyo.
Kileo ametumia mkutano huo kuiomba serikali kuongeza Bajeti ya Wizara ya Afya ili iendane na mahitaji ya kijinsia.