Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abeid Hallus, wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kujionea jinsi kituo cha mita za kushushia mafuta(flow meter)-Kurasini Oil Jet (KOJ) kilichopo Bandari ya Dar es Salaam kinavyofanya kazi.
.........
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo (Mb) ameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) kuhakikisha wanasimamia kikamilifu Flow Meter inayotumika kupima kiwango cha mafuta yanayoingia nchini ili Serikali ipate mapato halisi.
Ameyasema hayo alipotembelea na kukagua kukagua na kujionea jinsi kituo cha mita za kushushia mafuta(flow meter)-Kurasini Oil Jet (KOJ) kilichopo Bandari ya Dar es Salaam kinachosimamiwa na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA)
Aidha, Dkt. Jafo, amebainisha kuwa Bandari ya Dar es Salaam ndiyo lango kuu la kibiashara hapa nchini na Wakala wa Vipimo(WMA) wana jukumu la kujua kiwango cha mafuta kinachoingia nchini ili kuhakikisha Serikali inapata Pato halisi kutokana na mafuta hayo.
Aidha, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam na kuleta tija kubwa hususan ufungaji wa mitambo ya kisasa ya Flow Mita inayotumika kupima kiwango cha matufa yanayoingia nchini na kutatua changamoto iliyokuwepo muda mrefu katika upimaji wa mafuta hayo.
Pia alipongeza TPA kwa kazi kubwa ya kuboresha upakuaji na uondoaji wa mizigo katika bandari hiyo hali inayorahisisha ufanyaji biashara nchini kwa kupunguza siku za upakuaji mizigo inayoingia nchini..
Naye Kaimu MKurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bwana Abeid Garus ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa Uwekezaji na vifaa ambavyo vimeongeza ufanisi ambapo alibainisha kuwa awali meli ilikuwa ikitumia siku saba kupakua mzigo lakini kwa sasa inatumia siku tatu tu hadi nne. Aidha, aliongeza kuwa Idadi ya siku za meli kusubiri kuingia bandarini awali ilikuwa hadi siku 30 kwa sasa zinasubiri siku tano hadi siku saba hali ambayo inachagiza ubireshaji wa utoaji huduma na utendaji
Naye Afisa Vipimo Mwandamizi wa WMA katika bandari hiyo, Bwana Tegemeo Cosmas, amebainisha kuwa kwa sasa Flow Meter zinahakikiwa kila mwaka na zinapima mafuta kwa usahihi mkubwa.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abeid Hallus, wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kujionea jinsi kituo cha mita za kushushia mafuta(flow meter)-Kurasini Oil Jet (KOJ) kilichopo Bandari ya Dar es Salaam kinavyofanya kazi,.
Social Plugin