MAIN FM YAPULIZA KIPENGA CHA BODABODA CUP KIGOMA


Washindi katika mechi ya ufunguzi kombaini ya Bodaboda Mlole (jezi nyeupe) na Kombaini ya bodaboda Bangwe jezi za bluu
Mwakilishi wa kampuni ya gesi ya kupikia ya Oryx, Gibson  Rodgers (kulia) akikabidhi mtungi wa gesi kwa mchezaji wa kombaini ya Bodaboda Mlole ambaye alikuwa mchezaji bora wa mechi ya ufunguzi
Pascal Willian Mkurugenzi wa Main FM akizungumza na waandishi baada ya mechi ya ufunguzi
Dolla Buzaire Afisa Tawala wa wilaya Kigoma aliyemwakikisha Mkuu wa wilaya Kigoma

Na Editha Karlo,Kigoma
 
TIMU nane za waendesha pikipiki (Bodaboda) zimeanza kupambana katika ligi maalum kwa ajili ya kuhamasisha masuala ya usalama barabarani na masuala ya afya ya uzazi huku Mshindi wa mashindano hayo akitarajia kuibuka na kitita cha shilingi milioni moja.


Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha Main FM ambao ndiyo waandaji wa mashindano hayo, Pascal Willian alisema kuwa mashindano hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Radio hiyo, jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa Kigoma na Hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni na kubainisha  kuwa mashindano hayo pia yatatumika kuhamasisha masuala ya uwekezaji.
  
 
Kipenga cha mashindano hayo kimepulizwa na Mkuu wa wilaya Kigoma,Dk.Rashid Chuachua ambaye aliwakilishwa na Afisa Tawala wa wilaya Kigoma Dola Buzaire ambaye alisema kuwa mashindano hayo yana maana kubwa katika kuhimiza usalama barabarani lakini pia kuhimiza suala la watu kufanya mazoezi na kushiriki michezo.
 
Katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Kawawa Ujiji mjini Kigoma timu ya kombaini ya Bodaboda Mlole imeifunga Kombaini ya bodaboda ya Bangwe kwa jumla ya Magoli 5 – 1.
 
Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo Mwakilishi wa kampuni ya gesi ya kupikia ya Oryx, Gibson Rodgers alisema kuwa kampuni hiyo itakuwa ikitoa mtungi mdogo wa gesi kwa kila mchezo kwa mchezo bora wa mechi ikiwa ni sehemu ya udhamini wao wa mshindano hayo kuchochea vijana kujituma zaidi uwanjani.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post