YALIYOJIRI WAKATI WA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2024, HITIMISHO WIKI YA VIJANA, KUMBUKIZI YA MIAKA 25 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA JK. NYERERE

YALIYOJIRI WAKATI WA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2024, HITIMISHO WIKI YA VIJANA NA KUMBUKIZI YA MIAKA 25 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE, LEO OKTOBA 14, 2024 JIJINI MWANZA

Aliyosema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

# Tumekuja Mwanza kwa ajili ya matukio matatu, ambayo ni kuhitimisha Wiki ya Vijana, kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024.

# Naipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu pamojana na Wizara ya Habari,  Utamaduni,  Vijana na Michezo Zanzibar kwa kuratibu shughuli hizi ambazo tunazikamilisha leo, wamefanya kazi kubwa.

# Nawapongeza vijana sita walioongoza mbio za Mwenge wa Uhuru nchi nzima, mmehamasisha umoja, upendo, mshikamano na amani nchini.

# Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere,
maono na fikra zake zimeendelea kuishi hata baada ya kifo chake, aliweza kutuunganisha na kudumisha amani, tukaongea lugha moja kwa upendo tukiwa makabila zaidi ya  120.

# Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikuwa na falsafa ya kupenda usawa na alichukia ufisadi, rushwa, chuki na dharau kwa binadamu. Hili ndiyo chimbuko la Mwenge wa Uhuru nchini kwetu.

# Mwenge wa Uhuru una historia ndani ya nchi yetu  na historia hiyo haiwezi kutenganishwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, ndiyo maana leo tumezindua kitabu chenye historia ya Mwenge wa Uhuru ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere, tukisome kitabu hiki na kuendeleza tunu ya Mwenge katika Taifa letu. 

# Tutunze mazingira, shughuli za binadamu tuzisimamie vema ili tuepuke athari za kuharibu mazingira, ambayo ni ukame na mabadiliko ya tabianchi. Mamlaka husika za mazingira simamieni kanuni ili tutunze na kuhifadhi mazingira.

# Tumepokea maoni na ushauri kutoka  kwa wakimbiza Mwenge, Serikali itaanza kuyafanyia kazi kwa maslahi ya nchi yetu.

# Novemba 27, 2024, ni Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini kote, tumieni fursa hii kila mwenye sifa kugombea na  kupiga kura ili kuchagua viongozi tunaowapenda na  watakaotutumikia kiutawala, hii ndiyo dhana ya kujitawala na kukuza demokrasia. Tuanze kwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu.

# Serikali inatambua changamoto baadhi zinazowakabili vijana, kwa ushirikiano ndani ya Serikali tunaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha tunaziondoa changamoto hizo ili mfanye shughuli zenu vizuri.

# Vijana tambueni kuwa, dunia na nchi yetu kuna changamoto kadhaa dhidi yenu ikiwemo; madawa ya kulevya, hivyo kuweni makini jiepushe nayo, jikinge na maradhi hasa UKIMWI, fanyeni michezo na mazoezi pamoja na lishe bora ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.

# Tunaendelea kukamilisha mradi mkubwa wa chanzo cha maji Butimba kwa gharama za shilingi bil. 71, na ukikamilika utatoa lita milioni 48 ambazo zitaondoa changamoto ya maji kwenye maeneo ambayo hakuna maji Mwanza.

# Ukamilishaji wa soko kuu la Mwanza unaendelea, naagiza mradi huu ukamilike  ifikapo Disemba mwaka huu, ili wafanyabiashara waendelee kufanya biashara zao vizuri.

# Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka Mwanza umefikia asilimia 60, tunadhamiria reli ya kisasa inafika Mwanza kwa wakati ili kurahisisha masuala ya usafiri na usafirishaji, huku Meli ya Mv Mwanza ambayo ni kubwa kuliko zote kwenye Ziwa Victoria iko kwenye hatua za ukamilishaji.

# Ujenzi wa vivuko unaendelea mkoani Mwanza, naahidi kuleta fedha zinazopelea hivi karibuni kuwezesha kazi kumalizika ili vivuko vianze kufanya kazi.

# Jengo la kusubiria abiria unaendelea katika uwanjawa ndege Mwanza,  Mamlaka ya viwanja vya ndege simamieni kwa uharaka ili jengo likamilike.

# Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi umefikia hatua za mwisho kukamilika, daraja limefikia asilimia 93, miundo mbinu mingine kama barabara zinaendelea vema, lengo ni kuifungua Mwanza na Tanzania kwa ujumla. 

# Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 zitazinduliwa  mkoani Pwani na kuzimwa mkoani Mbeya ambapo ndiyo mkoa utakaofanyika shughuli za kilele cha mbio za Mwenge.

Aliyosema Rais wa Serikali ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi

# Mwenge umekimbizwa mikoa yote Tanzania, umehamasisha maendeleo, ushirikiano na muungano wa Watanzania, Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. 

# Tunaahidi umoja, amani na upendo, tunaunga mkono jitihada zako Mhe. Rais unazozifanya ili tuwe na umoja katika nchi yetu.

# Tunatoa wito kwa Watanzania kutunza mazingira na kujitokeza kwa wingi kwenye kujiandikisha na kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024.

Aliyosema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa

# Tunakushukuru Rais wetu kwa kuendeleza tunu ya Taifa ambayo ni Mwenge wa Uhuru, tumefikia kilele leo, na kila sehemu Mwenge ulipopita umekumbusha umuhimu wa amani kwa maendeleo ya Taifa letu.

# Ujumbe mkuu wa Mbio za Mwenge mwaka 2024 ulijikita kwenye uhifadhi wa mazingira na uhamasishaji ushiriki wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Aliyosema Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda

# Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mwanza, ikiwemo; ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama vile daraja la Kigongo Busisi, reli ya kimataifa (SGR), na miradi ya maji.

Imeandaliwa na Idara ya Habari - (MAELEZO)


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post