Nabii Msambaratishaji 'Happy Shamawele' amesema hana mpango wa kuolewa!!
"Nimeshika neno la Mungu katika kitabu cha 1 Wakorintho 7, 8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. 1 Wakorintho 7
,9 Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa",amesema Nabii Msambaratishaji.
Anasema neno ndio hilo ndoa ni kwa sababu ya tamaa tu za mwili na walioko kwenye ndoa ni kwa sababu ya tamaa tu.
"Hivyo unaweza ukawa single na ukamtumikia Mungu kwa uaminifu kabisa kwani uliwahi kusoma popote kwenye biblia imeandikwa mke wa nabii Elia au nabii Elisha au nabii Musa hata ushawahi kuona mke wa mtume Paulo lakini walimtumikia Mungu kwa uaminifu na walikuwa watumishi wa Mungu wenye nguvu na walifanya kazi ya Mungu kwa viwango vya juu sana",amesema.
"Wakati mwingine ndoa zinaweza kuchelewesha maono yako maana wito ni wa mtu mmoja na maono ni yake mambo ya kukaa kusubiri mjadiliane kama wana ndoa, wakati mwingine unaweza kupotoshwa na mwenza wako maana uonavyo wewe sivyo aonavyo yeye mfano mzuri Samson alipokuwa na Delila ndipo likawa anguko lake",anaongeza Nabii Msambaratishaji.
"Sisemi watu wasiolewe au wasioe, ukiona huwezi kukaa pekee yako yaani single olewa tu, au oa tu",anasisitiza.
"Kingine watu wamekuwa wakihoji juu ya jina langu Nabii Msambaratishaji kama vile wanapata utata hapana hili jina ni kulingana na wito wangu jinsi nilivyoitwa na Mungu ni kusambaratisha kazi za shetani yaani ufalme wa giza na kuhakikisha ya kwamba ufalme wa Mungu aliye hai unainuliwa",anaeleza.
Nabii Msambaratishaji Happy Shamawele anapatikana kupitia simu namba +255755363504
Facebook Nabii Msambaratishaji Happy Shamawele
Instagram NABII MSAMBARATISHAJI HAPPY SHAMAWELE
Social Plugin