WAYDS,GAET,TGNP WAIPONGEZA SERIKALI NA WANANCHI UBORESHAJI MIUNDOMBINU ZAHANATI YA NGUNGA KISHAPU

NA SUMAI SALUM - KISHAPU

Shirika lisilokuwa la kiserikali WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) linalotekeleza mradi wa  Uwajibikaji Ufuatiliaji wa Kijamii (SAM) limeipongeza serikali Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kwa utekelezaji wa mapendekezo ya changamoto zilizoibuliwa mwaka Jana (2023)  kwenye zahanati ya Kijiji cha Ngunga Kata ya Talaga.

Akisoma taarifa ya mrejesho wa ufuatiliaji tathmini hiyo Leo Oktoba 31,2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwenye kikao kilichohusisha wadau mbalimbali wa maendeleo Charles Deogratius Mkurugenzi na Mratibu wa ufuatiliaji mradi wa SAM kutoka WAYDS mkoani Shinyanga amesema kuwa serikali imesaidia kwa asilimia 80 utekelezwaji wa mapendekezo waliyoibua   kuhusiana na changamoto mbalimbali zilizopo katika zahanati ya Ngunga.

"Tulifanya uchambuzi wa kina na kuangalia nyaraka za halmashauri tukaangalia budget,planning, matumizi na fedha na maelekezo yake ila specifically suala la afya tukatembelea hospitali ya Dr.Jakaya Kikwete kisha zahanati ya Ngunga na kuangalia kama wananchi wanashirikishwa kwenye mchakato wote, Kwa awamu hii hatujafanya hayo ya mwaka 2023 isipokuwa tulikuja kuangalia mapendekezo ya changamoto tulizoibua", amesema Deogratius.
Charles Deogratius

Ameongeza kuwa baada ya kutoa mapendekezo ya kushughurikia changamoto hizo waliunda kamati yenye jumla ya wajumbe sita wakiwemo mwakilishi kutoka WAYDS 1,Mwakilishi kutoka GAET,Maendeleo ya jamii,mipango,afya na mwenyekiti kamati ya huduma za jamii elimu afya na maji Halmashauri. 

Deogratius amesema walizingatia mambo matano katika kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo hayo ikiwa ni pamoja na Mipango na mgawanyo wa raslimali,Usimamizi wa matumizi,Usimamizi wa utendaji na ufanisi,Usimamizi wa uadilifu pamoja na Usimamizi wa uadilifu na  Usimamizi wa uwajibikaji.

"Tulitambua huduma ya kujifungua ilikuwa hakuna, huduma ya kulazwa wagonjwa, kukosekana samani ikiwemo viti,meza na makabati ya kutunzia dawa,ukosefu wa maji safi na salama na yanafaa kwa matumizi ya usafi wa zahanati tu, mganga mmoja na muuguzi mmoja", ameongeza.
    
MAFANIKIO

Deogratius amesema  huduma ya Kuzalisha ipo kwa sasa,ongezeko la uagizaji dawa,zahanati sasa inatoa huduma ya kupumzisha wagonjwa,zahanati imeshirikisha wananchi na kupata baadhi ya samani kutoka kwao na kwenye kituo cha afya jirani, uwepo mfumo wa uvunaji maji ya mvua.

Aidha mratibu ufuatiliaji SAM amesema bado zipo baadhi ya  changamoto ambazo hazijashughulikiwa ikiwemo upatikanaji wa samani,upungufu wa watoa huduma ya afya,kukosekana kwa mafuta ya watu wenye ulemavu katika zahanati  ya Ngunga,sanduku la maoni kutokuwa na ubora unaozingatia usiri.

Aidha akitoa mapendekezo kuhusu uboreshaji upatikanaji  watoa huduma za afya Mkurugenzi GAET Bi. Catherine Kalinga amesema iko haja ya halmashauri kutangaza nafasi za kujitolea kwa wahitimu wa sekta ya afya hasa wazawa wa maeneo husika.
Catherine Kalinga

"Nimeona kwa baadhi ya hospitali wao uruhusu watu wa kujitolea kisha wakati wanajenga na kuimarisha ujuzi wawashirikishe wadau mbalimbali wa maendeleo (Ngo's) ili watakapohitaji wahudumu wa afya wapewe kipaumbele watu hao kwanza", ameongeza Kalinga.

Hata hivyo akichangia utoaji mapendekezo kuhusu usogezwaji huduma ya upatikanaji mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi mratibu vituo vya taarifa na maarifa Wilaya ya Kishapu Fredina Said ameshauri serikali kusogeza katika vituo na zahanati ili kuwawezesha watumiaji kupata kwa urahisi na pia itasaidia jamii isiyotambua huduma hiyo kupata elimu.

Akijibu hoja Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Joseph Swalala amekiri kuwepo kwa mapungufu mbalimbali na kuahidi yaliyondani ya uwezo wa Halmashauri wataendelea kuyashughulikia huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali ikiwemo TGNP na wadau wengine kuunga mkono katika kutatua changamoto hizo.
Joseph Swalala

Aidha mganga mkuu wa Wilaya Dkt. Joseph Bahati amesema kuhusu samani watalishughulikia na fedha za CSR, ifikapo Novemba watakamilisha boksi la maoni linalozingatia usiri na ubora.

"Tunazo zahanati sita zilizokamilika tumeshindwa kuzifungua kwa sababu ya upungufu wa watoa huduma hivyo tunaomba wadau wetu TGNP watusaidie pia ikiwezekana kujenga nyumba za watumishi wetu wa zahanati na hata vituo vya afya na kuhusu suala la upatikanaji mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi halina tatizo watawasiliana ba mganga wao mfawidhi na atawapa taratibu zote lengo kila wananchi anufaike na upatikanaji huduma Bora za afya" , ameongeza Dr Bahati.

Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya huduma  za jamii,afya na maji na Diwani wa Kata ya Talaga Mhe. Richard Dominico amewashukuru TGNP, WAYDS,GAET, jeshi la akiba(sungusungu),wananchi pamoja na serikali kwa kushirikiana kuhakikisha wanaboresha na  kuimarisha huduma ya afya katika kijiji cha Ngunga.

"Ni kweli TGNP kupitia mradi wa SAM wamesaidia hata kuwajengea uwezo wananchi wa Ngunga ila elimu zaidi inahitajika ya ushirikishwaji katika shughuli mbalimbali za maendeleo hasa ya afya ili wawe tayari kutoa muda na hata fedha zao kusaidia kuondoa changamoto mbalimbali zilizobakia", amesema Mhe. Dominico
Mkurugenzi na Mratibu wa ufuatiliaji SAM mkoa wa Shinyanga kutoka WAYDS Charles Deogratius akiwasilisha taarifa ya mrejesho wa ufuatiliaji tathimini wa mapendekezo ya changamoto zilizopo zahanati ya Ngunga Kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Leo Oktoba 31,2024  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mradi wa ufuatiliaji uwajibikaji kijamii SAM unaotekelezwa na WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya TGNP - Picha na SUMAI SALUM 
Eva Salum (52) Mwakilishi wa wanawake/wananchi akizungumza kwenye kikao cha utoaji mrejesho wa ufuatiliaji tathimini wa mapendekezo ya changamoto zilizopo zahanati ya Ngunga Kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mradi wa ufuatiliaji uwajibikaji kijamii SAM unaotekelezwa na WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya TGNP 
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Swalala akizungumza kwenye kikao cha utoaji mrejesho wa ufuatiliaji tathimini wa mapendekezo ya changamoto zilizopo zahanati ya Ngunga Kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Leo Oktoba 31,2024  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mradi wa ufuatiliaji uwajibikaji kijamii SAM unaotekelezwa na WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya TGNP

Mkurugenzi GAET, Catherine Kalinga  akizungumza kwenye kikao cha utoaji mrejesho wa ufuatiliaji tathimini wa mapendekezo ya changamoto zilizopo zahanati ya Ngunga Kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Leo Oktoba 31,2024  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mradi wa ufuatiliaji uwajibikaji kijamii SAM unaotekelezwa na WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya TGNP 
Deogratius Musambi (78) Mwakilishi wa wazee akizungumza kwenye kikao cha utoaji mrejesho wa ufuatiliaji tathimini wa mapendekezo ya changamoto zilizopo zahanati ya Ngunga Kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mradi wa ufuatiliaji uwajibikaji kijamii SAM unaotekelezwa na WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya  TGNP 
Mganga Mfawidhi zahanati ya Ngunga kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Dr. Ramadhani Jogoro akisikiliza taarifa ya mrejesho wa mapendekezo yaliyopendekezwa kupitia mradi wa SAM unaotekelezwa na  shirika la WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya  TGNP  leo Oktoba 31,2024 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halamashauri hiyo.
Mwakilishi wa Diwani viti maalumu kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani  Shinyanga, Mhe.Felister Yahula  akizungumza kwenye kikao cha utoaji mrejesho wa ufuatiliaji tathimini wa mapendekezo ya changamoto zilizopo zahanati ya Ngunga Kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Leo Oktoba 31,2024  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mradi wa ufuatiliaji uwajibikaji kijamii SAM unaotekelezwa na WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya TGNP mkoani Shinyanga huku akiishauri TGNP kuzunguka vijiji vyote vya Tanzania ili wananchi wanufaike na keki ya taifa kwa pamoja.
Regina Edward (36) Mwakilishi wa kundi la watu wenye ulemavu akizungumza kwa furaha baada ya kusikia kusogezewa huduma ya upatikanaji mafuta ya wenye ulemavu wa ngozi kwenye kikao cha utoaji mrejesho wa ufuatiliaji tathimini wa mapendekezo ya changamoto zilizopo zahanati ya Ngunga Kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mradi wa ufuatiliaji uwajibikaji kijamii SAM unaotekelezwa na WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya TGNP.
Mtendaji wa Kijiji cha Ngunga Mussa Chacha akizungumzia maendeleo ya uwepo wa ulinzi katika zahanati hiyo kuwa unaendelea vizuri wakingoja uchaguzi wa serikali za mitaa kukamilika mwezi Novemba 27, 2024 kwenye kikao cha utoaji mrejesho wa ufuatiliaji tathimini wa mapendekezo ya changamoto zilizopo zahanati ya Ngunga Kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mradi wa ufuatiliaji uwajibikaji kijamii SAM unaotekelezwa na WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya TGNP 

Mganga mkuu Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Dk. Joseph Bahati akizungumza kwenye kikao cha utoaji mrejesho wa ufuatiliaji tathimini wa mapendekezo ya changamoto zilizopo zahanati ya Ngunga Kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Leo Oktoba 31,2024  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mradi wa ufuatiliaji uwajibikaji kijamii SAM unaotekelezwa na WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya Mtandao wa Jinsia TGNP Mkoani humo.
Mwenyekiti wa kamati ya huduma  za jamii Elimu,Afya na maji na Diwani wa kata ya talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Richard Dominico akizungumza kwenye kikao cha utoaji mrejesho wa ufuatiliaji tathimini wa mapendekezo ya changamoto zilizopo zahanati ya Ngunga Leo Oktoba 31,2024  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia mradi wa ufuatiliaji uwajibikaji kijamii SAM unaotekelezwa na WAYDS kwa kushirikiana na GAET chini ya TGNP 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post