MHANDISI MIHAYO AENDELEZA KAMPENI YA "NI RAHISI SANA" KUIMARISHA USALAMA MTANDAONI

Meneja wa TCRA Kanda ya Kaskazini Mhandisi Francis Mihayo (kulia) akiwa katika kituo cha redio cha Arusha One FM Radio 101.7 FM kilichopo jijini Arusha kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi na salama ya mtandao pamoja na kuhabarisha umma juu ya Kampeni ya Ni Rahisi Sana.

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Katika juhudi za kuimarisha uelewa wa umma kuhusu usalama mtandaoni, Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya KaskaziniMhandisi Francis Mihayo amefanya mahojiano katika kituo cha Redio cha Arusha One FM 101.7 FM. 

Katika mazungumzo hayo, Mhandisi Mihayo amezungumzia kampeni mpya ya "Ni Rahisi Sana," ambayo inatoa mwangaza kuhusu matumizi sahihi na salama ya mtandao.

Mhandisi Mihayo amefafanua kwamba kampeni hii ni mpango wa elimu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, unaokusudia kuongeza uelewa wa umma kuhusu hatari zinazoweza kuwakabili watumiaji wa mtandao. 

“Lengo kuu la kampeni hii ni kuhakikisha kwamba watumiaji wanapata uelewa wa kina kuhusu hatari za mtandaoni na jinsi ya kujilinda,” amesema.

Amebainisha kuwa, Kampeni ya "Ni Rahisi Sana" inalenga kuwahimiza Watanzania kujilinda dhidi ya uhalifu mtandaoni.

 Mhandisi Mihayo amesisitiza kuwa mazingira salama mtandaoni ni muhimu kwa kufikia malengo ya uchumi wa kidijitali. 

Mhandisi Mihayo amesisitiza umuhimu wa elimu na uelewa katika kujiweka salama mtandaoni.

 Kampeni ya "Ni Rahisi Sana" inatoa fursa kwa watanzania wote kujifunza jinsi ya kutumia teknolojia kwa usalama, na hivyo kuweza kufaidika na fursa zinazotolewa na uchumi wa kidijitali.

Kampeni hii ni hatua muhimu katika kujenga jamii yenye uelewa wa kina kuhusu usalama mtandaoni na inasaidia kuunda mazingira salama kwa kila mtumiaji. Ulinzi wa taarifa zetu ni jukumu letu sote!


 "Kauli mbiu ya kampeni ya Ni Rahisi sana itakuwa inasisitiza mambo mbalimbali mfano;

👉Ni rahisi sana kumtambua tapeli kwani atakupigia namba ya kawaida badala ya namba 100;

👉Ni rahisi sana kutoa taarifa kwa mtu anayetaka kukutapeli tuma namba yake kwenye namba 15040;

👉Ni rahisi sana kuwasiliana na TCRA endapo una malalamiko yanayomuhusu mtoa huduma wako au ukitaka kupata elimu au ushauri wa kutaka kuanzisha biashara ya mawasiliano piga namba ya bure 0800008272;

👉Ni rahisi sana kujua maudhui mtandaoni yanayolenga kupotosha 

👉Ni rahisi sana kujua habari feki;

👉Ni rahisi sana kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo kuanzisha club za Kidijitali;

👉Ni rahisi sana kujisajili na kuanza kutumia Kikoa cha DOT TZ;

👉Ni rahisi sana kwa wabunifu wote katika nyanja za TEHAMA kupata kupata rasilimali kama namba na masafa kwaajili ya kufanyia majiribio bunifu zao;

👉Ni rahisi sana kuhuisha mifumo ya kifaa cha mawasiliano

👉Ni rahisi sana kusoma vigezo na masharti 

👉Ni rahisi sana kuchukua tahadhari kwa watoto wetu wanapotumia mitandao

👉Ni rahisi sana kujilinda dhidi ya majaribio ya udukuzi 

👉Ni rahisi sana kutambua usahihi wa taarifa

👉Ni rahisi sana kutambua vyanzo vya habari 

👉Ni rahisi sana kujielimisha na kusoma zaidi 

👉Ni rahisi sana kutumia teknolojia kuhakiki taarifa mtandaoni.

#nirahisisana #cybersecurity #Cybersecurityawarenessmonth #secureourworld #tcratz #elimukwaumma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post