MIFUMO YA TAASISI 7 IMEANZA KUSOMANA

Katika mwaka 2023/24, Kituo cha Uwekezaji kimekamilisha ujenzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Kuhudumia Wawekezaji (Tanzania Electronic Investment Window - TeIW) kwa awamu ya kwanza ambao ulizinduliwa Septemba, 2023.

Mfumo huo umeunganishwa na mifumo ya Taasisi saba (7) ambazo ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji, Idara ya Kazi, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na TIC.

Mfumo huo, unamuwezesha mwekezaji kusajili mradi popote ndani na nje ya nchi na kupata vibali vya uwekezaji ndani ya siku 3 ikiwa ametimiza vigezo.

 Awamu ya pili ya ujenzi wa  mfumo huo itahusisha uunganishaji wa Taasisi nyingine saba (7) ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Kilimo, Tume ya Madini na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA). 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post