Maandamano yaliyoanzia viwanja vya Shirecu,ofisi ya mtendaji kata ya Kishapu kisha kumalizikia ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo wagombea nafasi za uenyeviti wa mitaa Kata ya Kishapu wakienda kuchukua fomu ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa serikali yakiongozwa na mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu Janipher Juma - Picha na Sumai Salum
Mwenyekiti Mpya wa UVCCM Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga aliyechaguliwa Jana na wanachama wa Chama hicho Jeniphe Juma akizungumza Leo Oktoba 28 ,2024 na wanaCCM kwenye viwanja vya ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi Kata ya Kishapu kwenye tukio la uchukuaji fomu za kugombea serikali za Mtaa.
Na Sumai Salum - Kishapu
Wagombea saba nafasi ya Mwenyekiti wa serikali za mitaa kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wamechukua fomu za serikali za kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu.
Zoezi hilo limefanyika Leo Oktoba 28,2024 likiambatana na maandamano ya kutembea kwa miguu kuanzia viwanja vya Shirecu kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi kisha kumalizikia katika viwanja vya ofisi ya Ccm Wilaya huku mwenyekiti mpya wa UVCCM Jenipher Juma na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Joel Ndettoson wakiongoza maandamano hayo na
Akizungumza baada ya uchukuaji fomu hizo mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu Jenipher Juma amewataka wagombea na wanaCCM wote kuendelea kuwa watulivu wakingojea muda wa kampeni huku wakiendelea kuonesha umoja kama walivyoonesha kwa kuwasindikiza.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kishapu Mhe. Joel Ndettoson amewapongeza wagombea wote walioshiriki kugombea ndani ya Chama na kisha kupatikana baadhi watakaopeperusha bendera ya Chama hicho kuwa hayo yote ni maamuzi ya wanachama wenyewe wanachotakiwa kufanya ni kushirikiana,kuungana,kupendana na kusaidiana.
"Ndugu zangu Leo hii tunashuhudia ndugu zetu wagombea wamechukua fomu,wamejaza na kisha wamerudisha hivyo hapo baadae tutawafahamisha tarehe ya kuzindua zoezi zima la kampeni lakini tuonyeshe uzalendo kwa jamii huku tukielewesha umuhimu wa kupiga kura katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa" ,ameongeza Ndettoson
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi Kata ya Kishapu Godwin Everygist amesema kuwa zoezi la uchukuaji fomu za serikali litasitishwa mnamo tarehe 1 Novemba saa kumi kamili (1:00) jioni hivyo vyama vyote vya siasa vinavyogombea vihakikishe vinapeleka wagombea kuchukua fomu na kujaza kisha kurejesha kabla ya muda kuisha.
Wagombea Saba (7) waliotoka vitongoji Saba vinavyounda Kata ya Kishapu ni pamoja na Kitongoji cha Mwasele "B",Lugaba,Lyandu,Mhunze,Kishapu,Isoso pamoja na Mwabusiga na wote wamechukua fomu wamejaza na kisha wamerudisha.
Maandamano yaliyoanzia viwanja vya Shirecu,ofisi ya mtendaji kata ya Kishapu kisha kumalizikia ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo wagombea nafasi za uenyeviti wa mitaa Kata ya Kishapu wakienda kuchukua fomu ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa serikali yakiongozwa na mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu Janipher Juma
Mgombea uenyekiti wa mtaa (Lubaga) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Bw.Mahona Makaranga(kushoto) akikabidhi fomu ya ugombea kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kishapu Bw.Godwin Evsrygist(kulia)
Mgombea uenyekiti wa mtaa (Mwasele B) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Bw.Fabian Juma Makongo(kushoto) akikabidhi fomu ya ugombea kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kishapu Bw.Godwin Evsrygist(kulia)
Mgombea uenyekiti wa mtaa (Isoso) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Bw.Robert Nyahuma (kushoto) akikabidhi fomu ya ugombea kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kishapu Bw.Godwin Evsrygist(kulia)
Mgombea uenyekiti wa mtaa (Mwabusiga) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Bw. Charles Bugangali(kushoto) akikabidhi fomu ya ugombea kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kishapu Bw.Godwin Evsrygist(kulia)
Mgombea uenyekiti wa mtaa wa Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Bw. Meshack Kuyenza (kushoto) akikabidhi fomu ya ugombea kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kishapu Bw. Godwin Evsrygist(kulia) Leo Oktoba 28,2024
Mgombea uenyekiti wa mtaa (Lyandu) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Bw.Joseph Mabula(kushoto) akikabidhi fomu ya ugombea kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kishapu Bw.Godwin Evsrygist(kulia)
Katibu wa CCM Kata ya Kishapu Wilayani Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Bw. Cornel Zengo akizungumza Leo Oktoba 28,2024 kwenye zoezi la wagombea wa serikali za mitaa kuchukua fomu za serikali Wilayani humo.
Social Plugin