Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ATCL YASISITIZA UFANISI KWA WAHITIMU WA HUDUMA ZA NDEGE


WAHITIMU wa mafunzo ya uhudumu wa ndege na huduma kwa wateja wametakiwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya anga. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi, ametoa wito huo katika mahafali ya pili ya Chuo cha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL Training Centre) yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Oktoba 4, 2024.

Amesema sekta ya uchukuzi ni moja ya sekta iyotegemewa nchini kutokana na kuongezeka kwa ndege zinazofanya safari zake ndani na nje.

Aidha amesema ATCL ilianzisha chuo hicho kwa kuwasomesha wafanyakazi wake,baada ya kuona sekta hiyo inakua kwa kasi, hivyo iliamua kuwakaribisha watu kutoka taasisi nyingine.

“Tangu tuanze mafunzo hayo ya muda mfupi tayari wameshahitimu wataalamu 700 kutoka chuoni hapo,Tunajivunia kwa sababu wahitimu wa Chuo hiki wamekuwa ni mfano kwa kuigwa kwa weledi wanaouonesha wanapoajiriwa kwenye nafasi mbalimbali ndani na nje ya nchi, ”amesema Mhandisi Matindi.

Pamoja na hayo amesema licha ya chuo hicho kupokea wafanyakazi wa sekta ya usafiri, pia wanapokea wanafunzi wapya wanaohitaji kujifunza utaalamu huo.

Naye, Mkuu wa chuo hicho, Elly Nditile, amesema wahitimu 56 walimaliza mafunzo hayo ambayo yalianza Machi 4, mwaka jana.

Nditile amesema dhumuni la kuanzisha kwa chuo hicho ni baada ya kuona usafiri wa anga unaongezeka nchini.

Amesema kuongezeka kwa usafiri huo umesaidia kupatikana kwa ajira kwa vijana na kwamba, chuo chao kinatoa elimu ya kisasa yakiwemo mafunzo kwa vitendo .

“Tumepata ushuhuda kutoka taasisi mbalimbali ambazo wafanyakazi wao walipata elimu kutoka chuo hiki kuwa, utendaji wao wa kazi umekuwa vizuri tofauti ilivyokuwa awali,”amesema Nditile. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com